TOKA TFF: FDL – MAKUNDI MSIMU MPYA 2017/18 YAPANGWA!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TFF TOKA SITJULAI 26, 2017

MAKUNDI LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU 2017/18

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19.

Kwa mujibu wa makundi hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Ligi ya TFF, kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.

Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.

Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya  Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

Kadhalika, TFF imeagiza timu za Ashanti United, Friends Rangers, KMC na Polisi Dar ya Dar es Salaam kuwasilisha majina ya viwanja vitakavyotumiwa na timu zao wakati wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.

Kutaja viwanja hivyo ni matakwa ya Kanuni ya 6 (1) za kanuni Mama ya VPL inayozungumzia Viwanja kadhalika kusomwa pamoja na Kanuni ya 11 inayozungumzia Leseni za Klabu kwamba kila timu haina budi kuwa na viwanja vya mcehi za nyumbani ikiwa ni masharti ya kupata leseni ya klabu.

……………………………………………………………..………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TOKA TFF: TENGA APONGEZWA, KOCHA STARS ALIA NA BAHATI KUTUPWA NJE RWANDA!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

JULAI 20, 2017

TFF YAMPONGEZA TENGA

TFF TOKA SITKaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia amempongeza Leodegar Chilla Tenga - Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.

“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka. 

Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.

“Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.

BAHATI HAIKUWA UPANDE WETU - KOCHA

Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Fulgence Novatus, amesema kwamba Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti  ya SBL haikuwa na bahati katika mchezo dhidi ya Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa Kigali ulioko kata ya Nyamirambo.

“Tumecheza vema, tulitafuta nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki mpira. Lakini kila tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema Novatus mara baada ya mchezo huo.

Matokeo ya sare tasa ya jana yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na Uganda mwezi ujao.

Pamoja na kushindwa kusonge mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza mechi 11 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.

……………………………………………………………..………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

 

CHAN: TAIFA STARS NJE, RWANDA KUIVAA UGANDA!

CAF 2Taifa Stars Leo imerudiana na Rwanda huko Kigali Stadium, Nyamirambo Nchini Rwanda katika Mechi ya Mashindano ya CHAN na kutoka 0-0 na hivyo kutupwa nje.

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Mjini Mwanza, Stars na Amavubi zilitoka 1-1 na sasa Rwanda wamesonga Raundi ya 3 kwa Bao la Ugenini.

Katika Raundi hiyo, Rwanda watacheza na Uganda ambayo imeibamiza South Sudan 5-1.

KANDA YA KATI-MASHARIKI:

-Kutoa Nchi 2 pamoja na Mwenyeji Kenya

**Eritrea imejitoa

***Nchi zitakazoshiriki:

-Burundi

-Djibouti

-Ethiopia

-Rwanda

-Somalia

-South Sudan

-Sudan

-Tanzania

-Uganda

Ratiba

Raundi ya Pili

Julai 14

South Sudan 0 Uganda 0

Julai 15

Tanzania 1 Rwanda 1

Djibouti 1 Ethiopia 5

Burundi v Sudan [IMEFUTWA]

Julai 21

Sudan v Burundi [IMEFUTWA]

Julai 22

Uganda 5 South Sudan 1 [Uganda yasonga, Jumla Bao 5-1]

Rwanda 0 Tanzania 0 [Rwanda yasonga kwa Bao la Ugenini, Jumla Mabao 1-1 kwa Mechi 2]

Julai 23

Ethiopia v Djibouti [Djibouti imejitoa]

**FIFA imeisimamisha Sudan na hivyo kufutwa Mashindano ya CHAN na Burundi kupata ushindi wa Chee

Raundi ya Tatu

Agosti 11

Uganda v Rwanda

Ethiopia v Burundi

**Marudiano Agosti 18

CAF YAPANUA AFCON, FAINALI KUWA NA TIMU 24!

>CHAN: TAIFA STARS JUMAMOSI KUIVAA AMAVUBI HUKO NYAMIRAMBO!

CAF 2CAF imeamua kuzipanua Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, kutoka Timu 16 na kuwa na Timu 24.

Fainali hizo zitafanywa kila baada ya Miaka Miwili na sasa zitachezwa Miezi ya Juni na Julai badala ya Januari na Februari ilivyo sasa.

Uamuzi huo wa CAF umefanywa kwenye Mkutano wa CAF uliofanyika Juzi huko Rabat, Morocco na unategemewa kupitishwa na Kamti Kuu ya CAF.

Kwenye Mashindano ya AFCON 2019, Tanzania ipo Kundi L na katika Mechi yake ya kwanza ilitoka 1-1 na Lesotho Mjini Dar es Salaam.

Timu nyingine kwenye Kundi hilo ni Uganda na Cape Verde ambao walipambana katika Mechi ya kwanza na Uganda kushinda.

Wakati huo huo, Taifa Stars Jumamosi itarudiana na Rwanda huko Kigali Stadium, Nyamirambo Nchini Rwanda katika Mechi ya Mashindano ya CHAN.

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Mjini Mwanza, Stars na Amavubi zilitoka 1-1.

Mshindi wa Marudiano hayo atachuana na Mshindi kati ya Uganda au South Sudan.

KANDA YA KATI-MASHARIKI:

-Kutoa Nchi 2 pamoja na Mwenyeji Kenya

**Eritrea imejitoa

***Nchi zitakazoshiriki:

-Burundi

-Djibouti

-Ethiopia

-Rwanda

-Somalia

-South Sudan

-Sudan

-Tanzania

-Uganda

Ratiba

Raundi ya Pili

Julai 14

South Sudan 0 Uganda 0

Julai 15

Tanzania 1 Rwanda 1

Djibouti 1 Ethiopia 5

Burundi v Sudan [IMEFUTWA]

Julai 21

Sudan v Burundi [IMEFUTWA]

Julai 22

Uganda v South Sudan

Rwanda v Tanzania [Refa: Brian Miiro [Uganda]]

Julai 23

Ethiopia v Djibouti

**FIFA imeisimamisha Sudan na hivyo kufutwa Mashindano ya CHAN na Burundi kupata ushindi wa Chee

Raundi ya Tatu

Agosti 11

South Sudan/Uganda v Tanzania/Rwanda

Djibouti/Ethiopia v Burundi

**Marudiano Agosti 18

TFF: WANAFAMILIA WANNE WALIOFUNGIWA WAFUTIWA ADHABU!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
JULAI 17, 2017
TFF TOKA SITTAARIFA YA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.

Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.

Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.

Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.

“Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema Tarimba.

Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.

“Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.

Kwa niaba ya TFF, Ofisa Habari wa Shirikisho, Alfred Lucas, wameyapokea mapendekezo hayo kutoka kwa Tarimba na kwamba tutafanyia kazi ili kurekebisha makosa hayo kwa manufaa ya soka la Tanzania.

……………………………………………………………..………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA