VPL: 1 LAWAPAISHA VINARA SIMBA 4 MBELE YA MABINGWA YANGA!

VPL-LOGO-MURUAVINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba, Leo huko Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wamezidi kupa kileleni baada ya kuifunga Ruvu Shooting 1-0.

Bao hilo la ushindi la Simba lilifungwa na Mohammed Ibrahim.

Matokeo hayo yanaiweka Simba Nambari Wani kwenye VPL wakiwa na Pointi 44 wakifuatia Yanga wenye Pointi 40 zote zikiwa zimecheza Mechi 18 kila mmoja.

Mechi nyingine ya VPL inachezwa Usiku huu huko Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa Timu za Yanga na Simba VPL inasitishwa kwao hadi baada ya kwisha Mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayochezwa huko Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13.  

VPL - Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Desemba 26

Ruvu Shooting 2 Tanzania Prisons 0

Jumatano Desemba 28

Yanga 4 Ndanda FC 0

Mtibwa Sugar 1 Majimaji FC 0

Alhamisi Desemba 29

Ruvu Shooting 0 Simba 1

Azam FC 1 Tanzania Prisons 0

Jumamosi Desemba 31

Mwadui FC v Kagera Sugar [Mwadui Complex, Mwadui]

African Lyon v JKT Ruvu [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]

Mbeya City v Mbao FC [Sokoine, Mbeya]

Jumapili Januari 1

Toto African v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]