MAPINDUZI CUP: SIMBA YAANZA, YAIBWAGA TAIFA JANG’OMBE!

>JUMATATU YANGA NA JAMHURI, AZAM NA ZIMAMOTO!

AMAAN-STADIUM-17LEO MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, ambayo yalianza Juzi kwa Mechi moja ya Kundi A, yameendelea huko Amaan Stadium, Zanzibar kwa Mechi nyingine mbili za Kundi A.

Katika Mechi ya kwanza Juzi Usiku, Timu pinzani huko Zanzibar zilipambana na Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0.

Katika Mechi ya kwanza ya hii Leo iliyochezwa mapema, KVZ ya Zanzibar ilichapwa 2-0 na URA ya Uganda, ambao ndio Mabingwa Watetezi, na Usiku, Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba, walitinga Amaan Stadium kwa kucheza na Taifa Jang’ombe.

Katika Mechi hiyo, Simba walipata Bao la Kwanza Dakika ya 27 ambalo Muzamil Yasin alifunga na kupiga la Pili Dakika ya 41 Mfungaji akiwa Juma Luizio.

Dakika ya 76, Lufungo wa Simba alijifunga mwenyewe na kuipa Taifa Jang’ombe Bao na kufanya Gemu iwe 2-1.

+++++++++++++++++

MAKUNDI:

KUNDI A

-Simba

-Taifa Jang;ombe

-Jang’ombe Boys

-KVZ

-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B

-Yanga

-Azam FC

-Jamhuri

-Zimamoto

+++++++++++++++++

Kesho Januari 2, Mechi za Kundi B zitaanza kwa Azam FC kucheza na Zimamoto kuanzia Saa 10 Jioni na Yanga kuivaa Jamhuri Saa 2 na Nusu Usiku.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni

Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku)

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys vs URA (Saa 10:00 jioni)

KVZ vs Simba (Saa 2:30 usiku)

Januari 4, 2017

Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)

Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017

KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.