MAPINDUZI CUP: MABINGWA URA WAPIGWA NA JANG’OMBE BOYS, SIMBA YAITUNGUA KVZ!

>JUMATANO NI ZIMAMOTO-YANGA, JAMHURI-AZAM!

AMAAN-STADIUM-17MABINGWA WATETEZI wa Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, URA ya Uganda Leo Jioni imebwagwa 2-1 na Jang’ombe Boys ya Zanzibar wakati Usiku Simba ikiitungua KVZ 1-0 katika Mechi za Kundi A.

Shujaa wa Jang’ombe Boys ni Hamis Mussa aliewafungia Bao zote 2 na kuwapa Pointi zao 2 za kwanza toka Kundi A la Mapinduzi Cup baada ya kupoteza Mechi yao ya kwanza walipofungwa 1-0 na Jirani zao Taifa Jang’ombe.

Nao URA ambao walishinda Mechi yao ya kwanza kwa kuichapa 2-0 KVZ sasa itabidi kugangamala watakapocheza na Simba Alhamisi Usiku ikiwa watataka kutetea vyema Taji lao.

Katika Mechi ya nyingine ya Kundi A Usiku huu, Bao la Dakika ya 44 la Mzamiru Yassin limewapa Simba ushindi wa 1-0 walipocheza na KVZ ya Zanzibar ambayo ilimaliza ikiwa na Mtu 10 baada ya Rashid Hussein Rashid kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 89.

Huo ni ushindi wao wa pili Simba na kuwafanya waongoze Kundi A wakiwa na Pointi 6.

+++++++++++++++++

MAKUNDI:

KUNDI A

-Simba

-Taifa Jang’ombe

-Jang’ombe Boys

-KVZ

-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B

-Yanga

-Azam FC

-Jamhuri

-Zimamoto

+++++++++++++++++

Jumatano zipo Mechi 2 za Kundi B kwa Yanga kucheza na Zimamoto na kisha Azam FC kuikwaa Jamhuri.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)

Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017

KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.