MAPINDUZI CUP: YANGA MOTO WABONDA TENA, WACHUNGULIA NUSU FAINALI!

AMAAN-STADIUM-17MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, yameendelea Leo kwa Timu inayotisha Yanga kupata ushindi wake wa pili wa Kundi B.

Hii Leo Yanga, ambao walianza kwa kishindo Kundi B kwa kuinyuka Jamhuri ya Pemba 6-0, wameichapa Zimamoto yay a Zanzibar 2-0 kwa Bao za Dakika za 11 na 21 za Simon Msuva.

Yanga, waliotawala Mechi hii, wangeweza kupata Bao la 3 walipopewa Penati kwenye Dakika ya 50 lakini Penati hiyo iliyopigwa na Simon Msuva ilichezwa na Kipa wa Zimamoto.

Matokeo haya yamewaweka Yanga kwenye nafasi nzuri mno ya kutinga Nusu Fainali ingawa kwa hali ilivyo unaweza tu kutamka tayari wapo Nusu Fainali.

Jumamosi Yanga watakamilisha Mechi zao za Kundi B kwa kucheza na Azam FC.

+++++++++++++++++

MSIMAMO:

KUNDI A

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

SIMBA

2

2

0

0

3

1

2

6

2

URA

2

1

0

1

3

2

1

3

3

JANG’OMBE BOYS

2

1

0

1

2

2

0

3

4

TAIFA JANG’OMBE

2

1

0

1

2

2

0

3

5

KVZ

2

0

0

2

0

3

-3

0

KUNDI B

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

YANGA

2

2

0

0

8

0

8

6

2

AZAM

1

1

0

0

1

0

1

3

3

ZIMAMOTO

2

0

0

2

0

3

-3

0

4

JAMHURI

1

0

0

1

0

6

-6

0

+++++++++++++++++

 

Baadae Usiku huu, Azam FC watacheza na Jamhuri na Alhamisi zipo Mechi 2 za Kundi A kati ya KVZ na Jang'ombe Boys Saa 10 Jioni na Usiku ni Simba na Mabingwa Watetezi URA.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto 0 Yanga 2

Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017

KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.