MAPINDUZI CUP: TAIFA JANG’OMBE YASHINDA, KUNDI A SASA HALI TETE, NANI KWENDA NUSU FAINALI, JANG’OMBE ZOTE 2 AU SIMBA AU URA?

>>JUMAMOSI YANGA, WALIOFUZU, NA AZAM FC INAYOSAKA KUFUZU!

AMAAN-STADIUM-17MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, yameendelea Jana kwa Mechi moja ya Kundi A iliyoleta utata mkubwa nani atafuzu kuingia Nusu Fainali.

Usiku huu, Taifa Jang’ombe imeipiga KVZ 3-1 na kujiweka hai kutinga Nusu Fainali wakiungana na Simba, Jang’ombe Boys na Mabingwa Watetezi URA ya Uganda kugombea nafasi 2.

Katika Mechi za mwisho za Kundi A hapo Jumapili Simba itacheza na Jang'ombe Boys na Taifa Jang'ombe kucheza na URA.

+++++++++++++++++

MSIMAMO:

KUNDI A

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

SIMBA

3

2

1

0

3

1

2

7

2

JANG’OMBE BOYS

3

2

0

1

5

3

2

6

3

TAIFA JANG’OMBE

3

2

0

1

5

3

2

6

4

URA

3

1

1

1

3

2

1

4

5

KVZ

4

0

0

4

2

9

-7

0

KUNDI B

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

YANGA

2

2

0

0

8

0

8

6

2

AZAM

2

1

1

0

1

0

1

4

3

JAMHURI

2

0

1

1

0

6

-6

1

4

ZIMAMOTO

2

0

0

2

0

3

-3

0

+++++++++++++++++

Jumamosi zipo Mechi 2 za mwisho za Kundi B ambalo Yanga tayari wametinga Nusu Fainali na kuacha kimbembe cha nani anaungana nao kwa Azam FC na Jamhuri ingawa Azam FC ndio wenye nafasi kubwa zaidi kufuzu.

Katika Mechi hizo, Yanga watacheza na Azam FC na Jamhuri kuivaa Zimamoto ambayo tayari ipo nje ya Mashindano.

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto 0 Yanga 2

Jamhuri 0 Azam 0

Januari 5, 2017

KVZ 1 Jang'ombe Boys 3

Simba 0 URA 0

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

Januari 7, 2017

Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)

Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku)

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)

Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.