MAPINDUZI CUP: JUMANNE NUSU FAINALI NI DABI YA KARIAKOO YANGA v SIMBA NA AZAM FC v TAIFA JANG’OMBE AU URA!

AMAAN-STADIUM-17Ingawa imebaki Machi 1 tu ya Kundi A la Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, lakini Nusu Fainali ishadhihirika kuwa Jumanne ni Bigi Mechi wakati Dabi ya Kariakoo ikihamia Amaan Stadium Zanzibar kwa Yanga kupambana na Watani zao Simba ambao Leo wamejikita huko baada ya kuichapa Jang'ombe Boys 2-0.

Bao za Simba hii Leo zilifungwa na Laudit Mavugo na kuhakikisha Simba ikimaliza Kundi A kuwa Washindi wa Kundi hilo na hivyo kucheza na Mshindi wa Pili wa Kundi B ambae ni Yanga baada ya Jana kuchapwa 4-0 na Azam FC.

Azam FC wamemaliza Washindi wa Kundi B na kusubiri Mpinzani wao wa Nusu Fainali ambae ataamuliwa kwa Mechi ya mwisho ya Kundi A Usiku huu kati ya Mabingwa Watetezi URA ya Uganda na Taifa Jang’ombe ya Zanzibar.

+++++++++++++++++

MSIMAMO:

KUNDI A

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

SIMBA

4

3

1

0

5

1

4

10

2

JANG’OMBE BOYS

4

2

0

2

5

5

0

6

3

TAIFA JANG’OMBE

3

2

0

1

5

3

2

6

4

URA

3

1

1

1

3

2

1

4

5

KVZ

4

0

0

4

2

9

-7

0

KUNDI B

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

AZAM

3

2

1

0

5

0

5

7

2

YANGA

3

2

0

1

8

4

4

6

3

ZIMAMOTO

3

1

0

2

2

3

-1

3

4

JAMHURI

3

0

1

2

0

8

-8

1

+++++++++++++++++

KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto 0 Yanga 2

Jamhuri 0 Azam 0

Januari 5, 2017

KVZ 1 Jang'ombe Boys 3

Simba 0 URA 0

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

Januari 7, 2017

Jamhuri 0 Zimamoto 2

Yanga 0 Azam 4

Januari 8, 2017

Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)

Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Azam FC v Taifa Jang’ombe/URA (Saa 10: 00 jioni)

Simba v Yanga (Saa 2:15 Usiku)

Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 30 usiku.