MAPINDUZI CUP: LEO PATASHIKA ZENJI, YANGA v SIMBA!

>>NI MARA YA 5 DABI YA KARIAKOO, DAR KUHAMIA UNGUJA!

>HISTORIA YA DABI HII MSHINDI NI YULE ANAECHANGA VIZURI ‘KARATA’ NDANI YA DAKIKA 90 ZA MECHI!

AMAAN-STADIUM-17LEO zipo Mechi Mbili za Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, lakini macho, masikio na kila hisia ni Bigi Mechi wakati Dabi ya Kariakoo ikihamia Amaan Stadium Zanzibar kwa Yanga kupambana na Watani zao Simba.

Nusu Fainali nyingine hii Leo ni kati ya Watoto wa Nyumbani Taifa Jang’ombe, waliowatoa waliokuwa Mabingwa Watetezi URA ya Uganda, na Azam FC.

Wakati Kambi ya Simba ni shwari baada ya kushinda Mechi 3 na Sare 1 kwenye Kundi A, Yanga kuna walakini baada kushinda Mechi zao 2 za kwanza za Kundi B kwa kishindo na kufuzu lakini wakatandikwa 4-0 na Azam FC katika Mechi yao ya mwisho ya kukamilisha Ratiba Kundini.

Msukukosuko huo umemfanya Kocha Mkuu wa Yanga kutoka Zambia, George Lwandamina, kukiri hali ni ngumu kwao na hasa kutokana na Majeruhi ambao wataikosa Mechi na Simba ambao ni Straika Amissi Tambwe kutoka Burundi, Wazambia wao Wawili, Justin Zulu na Obrey Chirwa, na Mzimbabwe Donald Ngoma.

Hata hivyo, Kocha huyo amesisitiza wataingia na kupigana kiume kwa Kikosi kilichobaki huku Historia ya Dabi hii ikidhihirisha Miaka nenda rudi Ubora wa Timu si kigezo kwani yeyote anaweza kushinda mtanange kati yao ikiwa Karata zitachangwa vizuri ndani ya Dakika 90 za Mechi.

Yanga na Simba zimekutana Amaan Stadium, Zanzibar mara 4.

Pata kumbukumbu:

-Mechi ya Kwanza 1975

Mwaka 1975, Yanga iliichapa Simba 2-0 kwenye Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa Bao za Gibson Sembuli na Sunday Manara.

-Mechi ya Pili 1992

Simba ilishinda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa Mikwaju ya Penati 6-5, baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 120 ambayo Simba ilitangulia kufunga kwa Bao la Hussein Masha na Yanga kurudisha kupitia Saidi Mwamba ‘Kizota’,

-Mechi ya Tatu 1992

Bao pekee la Daniel Kimti liliipa Simba ushindi wa 1-0 katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano.

-Mechi ya Nne 2011

Simba ilishinda 2-0 kwenye Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa Bao za Shija Mkina na Mussa Hassan ‘Mgosi;.

+++++++++++++++++

MAKUNDI

MSIMAMO:

KUNDI A

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

SIMBA

4

3

1

0

5

1

4

10

2

TAIFA JANG’OMBE

4

3

0

1

6

3

3

9

3

JANG’OMBE BOYS

4

2

0

2

5

5

0

6

4

URA

4

1

1

2

3

3

0

4

5

KVZ

4

0

0

4

2

9

-7

0

KUNDI B

NA

TIMU

P

W

D

L

F

A

GD

PTS

1

AZAM

3

2

1

0

5

0

5

7

2

YANGA

3

2

0

1

8

4

4

6

3

ZIMAMOTO

3

1

0

2

2

3

-1

3

4

JAMHURI

3

0

1

2

0

8

-8

1

+++++++++++++++++

­­KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto 0 Yanga 2

Jamhuri 0 Azam 0

Januari 5, 2017

KVZ 1 Jang'ombe Boys 3

Simba 0 URA 0

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

Januari 7, 2017

Jamhuri 0 Zimamoto 2

Yanga 0 Azam 4

Januari 8, 2017

Simba 2 Jang'ombe Boys 0

Taifa Jang'ombe 1 URA 0

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Azam FC v Taifa Jang’ombe (Saa 10: 00 jioni)

Simba v Yanga (Saa 2:15 Usiku)

Ijumaa, Januari 13, 2017

FAINALI

Saa 2: 15 Usiku

Azam FC/Taifa Jang’ombe v Simba/Yanga