KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: ENGLAND, MABINGWA WA DUNIA GERMANY ZAPETA!

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Machi 26

**Saa za Bongo

San Marino 0 Czech Republic 6 [Kundi C]

Armenia 2 Kazakstan 0 [Kundi E]

England 2 Lithuania 0 [Kundi F]

Azerbaijan 1 Germany 4 [Kundi C]        

21:45 Malta v Slovakia [Kundi F] 

21:45 Romania v Denmark [Kundi E]

21:45 Scotland v Slovenia [Kundi F]      

21:45 Northern Ireland v Norway [Kundi C]    

21:45 Montenegro v Poland [Kundi E]

++++++++

ENGLAND-DEFOE-WAYAHII LEO England wameendelea kupiga hatua kutinga Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuifunga Lithuania 2-0 Uwanjani Wembley London ikiwa ni Mechi ya Kundi F.

Baada ya Mechi 5, England wapo kileleni mwa Kundi F lenye Timu 6 wakiwa na Pointi 13 wakifuata Slovenia wakiwa na Pointi 8 kwa Mechi 4.

Baadae Usiku huu, Slovenia watakuwa Wageni wa Scotland katika Mechi ngumu mno ya Kundi F.

Bao za England hii Leo zilifungwa na Jermaine Defoe Dakika ya 21, likiwa Bao lake la kwanza tangu Novemba 2013 kwa England alipoichezea kwa mara ya mwisho, na la Pili kupigwa na Jamie Vardy, alieingizwa Dakika ya 60, na kupachika Bao hilo Dakika ya 66.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Kwenye Mechi nyingine za mapema hii Leo, Mabingwa wa Dunia Germany wamejiweka sawa kwenda Russia kwa kushinda Ugenini walipoicharanga Azerbaijan Bao 4-1 katika Mechi ya Kundi C na kuzidi kupaa kileleni.

Hadi Mapumziko, Germany waliongoza 3-1 kwa Bao za Andre Schurrle, Thomas Mueller na Mario Gomez huku Azerbaijan wakifunga kupitia Dimitrij Nazarov.

Germany walipata Bao la 4 Dakika ya 81 Mfungaji akiwa Andre Schurrle.

Baada ya Mechi 5, Germany wanaongoza Kundi C wakiwa na Pointi 15 na kufuata Czech Republic wenye Pointi 8.

VIKOSI:

England: Hart; Walker, Stones, Keane, Bertrand; Oxlade-Chamberlain, Dier; Sterling [Rashford, 60’], Alli, Lallana; Defoe [Vardy, 60’]

Lithuania:  Šetkus; Vaitkūnas, Kijanskas, Klimavičius, Slavickas; Kuklys, Žulpa; Novikovas [Grigaraviciu, 54’], Slivka [Paulius, 87'], Černych; Valskis [Matulevicius, 73']

REFA: Ruddy Buquet [France]

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba:

**Saa za Bongo

Ijumaa Juni 9

21:45 Bosnia And Herzegovina v Greece [Kundi H]

21:45 Netherlands v Luxembourg [Kundi A]

21:45 Belarus v Bulgaria [Kundi A]       

21:45 Latvia V Portugal [Kundi B]         

21:45 Sweden v France [Kundi A]        

21:45 Faroe Islands v Switzerland [Kundi B]   

21:45 Estonia v Belgium [Kundi H]       

21:45 Andorra v Hungary [Kundi B]      

21:45 Gibraltar v Cyprus [Kundi H]       

KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: JUMAPILI ENGLAND WAPO WEMBLEY NA LITHUANIA!

WC-2018-EURO-QJUMAPILI, England wako Nyumbani kwao kucheza na Lithuania ikiwa ni Mechi ya Kundi F la Ulaya la kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Baada ya Mechi 4 kwa kila Timu England ndio wanaongoza Kundi F lenye Timu 6 wao wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na Slovenia wenye 8 na Lithuania wapo Nafasi ya wakiwa na Pointi 5.

Kwenye Mechi hii na Lithuania, England wataongozwa na Kipa Joe Hart ambae ndie amepewa Utepe wa Kepteni kwa vile Kepteni Wayne Rooney hayumo Kikosini kwa vile ni Majeruhi na Gary Cahill, ambae ndie alikuwa Nahodha Juzi walipofungwa 1-0 na Germany, yupo Kifungoni kwa Mechi 1.

Mara ya mwisho kwa Joe Hart, Kipa wa Man City anaecheza kwa Mkopo huko Italy na Torino, kuwa Nahodha wa England ilikuwa ni 2015 walipofungwa 2-0 na Spain.

Jumapili itamkosa pia Sentahafu wa Man United Chris Smalling ambae ameumia na hilo pamoja na kukosekana Cahill kumeifanya England kubakiwa na Masentahau Watatu ambao ni John Stones wa Man City, Michael Keane wa Burnley na Ben Gibson wa Middlesbrough.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Takwimu

-England hawajafungwa Mechi yeyote Mchujo wa Mashindano makubwa kwa Mechi 33 sasa za Kombe la Dunia na EURO.

-Kwenye Kundi la EURO 2016, England iliifunga Lithuania mara 2, 4-0 hapo Wembley na 3-0 Ugenini.

-Pamoja na Germany, England ndio Timu pekee haijaruhusu kufungwa hata Bao 1 katika Mechi hizi za Makundi za Kombe la Dunia 2018.

Tathmini

KUNDI F

Kinara: England (Pointi 10)

Wa Pili: Slovenia (8)

Hali ilivyo hadi sasa

England, licha ya kuyumbishwa kwa mabadiliko ya Kocha katikati ya kampeni hii, bado wapo kileleni na katika Mechi yao ya mwisho waliwanyuka Mahasimu wao wa Jadi Scotland 3-0.

Slovenia, ambao walitoka 0-0 na England, wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 ya England na wapo Pointi 2 mbele ya Timu ya 3 Slovakia.

Matokeo muhimu

Slovakia 0-1 England, Slovenia 1-0 Slovakia, England 3-0 Scotland

Gemu zijazo

26 Machi 2017: England v Lithuania, Malta v Slovakia, Scotland v Slovenia

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Machi 25

20:00 Cyprus v Estonia [Kundi H]

20:00 Bosnia And Herzegovina v Gibraltar [Kundi H]  

20:00 Sweden v Belarus [Kundi A]        

20:00 Andorra v Faroe Islands [Kundi B]         

20:00 Switzerland v Latvia [Kundi B]

22:45 Luxembourg v France [Kundi A]  

22:45 Bulgaria v Netherlands [Kundi A] 

22:45 Belgium v Greece [Kundi H]        

22:45 Portugal v Hungary [Kundi B]

Jumapili Machi 26

19:00 San Marino v Czech Republic [Kundi C]  

19:00 Armenia v Kazakstan [Kundi E]   

19:00 England v Lithuania [Kundi F]

19:00 Azerbaijan v Germany [Kundi C]  

21:45 Malta v Slovakia [Kundi F] 

21:45 Romania v Denmark [Kundi E]

21:45 Scotland v Slovenia [Kundi F]      

21:45 Northern Ireland v Norway [Kundi C]    

21:45 Montenegro v Poland [Kundi E]

SPURS RUKSA WEMBLEY MECHI ZA NYUMBANI MSIMU UJAO!

>>KUPISHA KITU KIPYA WHITE HART LANE!

WHITEHARTLANE-MPYAMAOMBI ya Tottenham Hotspur kuutumia Uwanja wa Wembley Jijini London kwa Mechi zao za Nyumbani Msimu ujao yamekubaliwa.

Brent Council, Halmashauri ambayo Uwanja huo upo, imepitisha kwa Kura uamuzi wa kuiruhusu Spurs kutumia Wembley kwa Mechi zao 27 na kuruhusu Uwanja wote kujazwa Watu 90,000.

Spurs wamepewa hadi Machi 31 kuthibitisha matumizi hayo.

Hivi sasa Spurs wanajenga Uwanja wao mpya jirani na ule wa sasa White Hart Lane na ambao unatarajiwa kuwa tayari kutumika kwenye Msimu wa 2018/19.

Sasa Spurs wanatafakari kama waendelee kuutumia White Hart Lane kwa Msimu ujao na ule wa 2018/19 ili wahamie Uwanja Mpya Msimu wa 2019/20.

Spurs hawakutaka kuutumia Wembley huku wakiwekewa sharti la Uwanja kutojazwa na Halmashauri ya Brent ambayo baadhi ya Wajumbe wake walipinga Uwanja kujazwa wote kutokana na kuogopa vitendo vya kihuni vya Washabiki na pia kuzorotesha Usafiri wa Eneo lao.

Wajumbe hao walitaka Spurs waruhusiwe kutumia Wembley kwa ujazo wa Watu 61,000 tu na si 90,000 kama vile uwezo wa Wembley yenyewe.

Kukubaliwa kwa Spurs kucheza Mechi 27 tu kuna sharti kuwa Mechi zikizidishwa zaidi ya hapo basi hawataruhusiwa kuwa na Washabiki zaidi ya 50,835 kwa Mechi za ziada.

PODOLSKI AIGA RASMI GERMANY KWA KUIBAMIZA ENGLAND!

PODOLSKILUKAS PODOLSKI amestaafu rasmi kuichezea Timu ya Taifa ya Germany Jana kwa kuiongoza kama Nahodha na pia kufunga Bao pekee na la ushindi walipowafunga England 1-0 huko Signal Iduna Park Jijini Dortmund Nchini Germany.
Hicho kilikuwa kipigo cha kwanza kwa Meneja wa England Gareth Southgate katika Mechi zake 4 tangu ashike wadhifa Mwaka Jana kutoka kwa Sam Allardyce.

Bao hilo la Podolski lilifungwa Dakika ya 69 kwa kigongo toka nje ya Boksi na kumshinda Kipa wa England Joe Hart.

England walikosa Bao baada ya Adam Lallana kupigacPosti na Shuti la Dele Alli kuokolewa na Kipa wa Germany Marc-Andre ter Stegen kwenye Kipindi cha Kwanza ambacho England walikuwa juu.

VIKOSI:

Germany (4-2-3-1) Ter Stegen; Kimmich, Rudiger, Hummels, Hector; Weigl (Can 66), Kroos; Sane, Podolski (Rudy 84), Brandt (Schurrle 59), Werner (Muller 77)

England (3-4-2-1): Hart; Keane, Smalling (Stones 84), Cahill; Walker, Dier, Livermore (Ward-Prowse 83), Bertrand (Shaw 83), Lallana (Redmond 66), Alli (Lingard 71), Vardy (Rashford 70)

REFA: Damir Skomina (Slovenia)
Jumatano Machi 22
Matokeo:

Cyprus 3 Kazakhstan 1

Czech Rep 3 Lithuania 0

Scotland 1 Canada 1

Germany 1 England 0

KIMATAIFA KIRAFIKI: JUMATANO NI SIGNAL IDUNA PARK GERMANY v ENGLAND!

GERMANY-ENGLANDJUMATANO Usiku Uwanja maarufu huko Dortmund, Signal Iduna Park, Nyumbani kwa Klabu Kigogo Borussia Dortmund, ndio dimba la Wapinzani wa Jadi wa Kimataifa, Germany na England, watakapopambana kwenye Mechi ya Kirafiki.

Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki, pia Mechi hii itatumiwa na Mabingwa wa Dunia Germany kumuaga rasmi Mchezaji wao Lukas Podolski akistaafu kuichezea Nchi yake baada ya kupiga nao Gemu 130 na pia kutwaa nao Kombe la Dunia Mwaka 2014 huko Brazil.

Podolski, mwenye Miaka 31 na ambae sasa yupo huko Uturuki na Galatarasay, aliwahi kuichezea pia Arsenal na mwishoni mwa Msimu huu atahamia huko Japan kuichezea Vissel Kobe.

Mbali ya kumtumia Podolski ambae alistaafu rasmi Mwaka Jana baada ya EURO 2016 huko France, Kocha wa Germany Joachim Low amethibitisha kuwakosa Majeruhi Mesut Ozil, Julian Draxler na Mario Gomez.

Nayo England imekumbwa na Majeruhi kadhaa ikiwakosa Nahodha wao Wayne Rooney, Harry Kane na Daniel Sturridge na kubaki na Mafowadi Watatu tu.

Meneja wa England, Gareth Southgate, anao Mastraika Watatu tu ambao ni Jamie Vardy, Marcus Rashford na Jermain Defoe.

Takwimi Muhimu - Uso kwa Uso

-Germany wamefungwa Mechi zao 3 za mwisho dhidi ya England walizochezea kwao Nchini Germany wakipigwa 5-1 Mwaka 2001, 2-1 hapo 2008 na 3-2 Mwaka 2016.

-Mara ya mwisho kwa Nchi hizi kukutana Nchini Germany huko Mjini Berlin, Machi 2016, Germany iliongoza 2-0 na England kushinda 3-2

-Germany hawajahi kufungwa Mechi mfululizo na England tangu walipopigwa Mechi 7 mfululizo kati ya Miaka 1935 na 1966 [Gemu 5 za mwisho katika kipindi hicho, kati ya 1954 na 1966, walijulikana kama West Germany baada ya Nchi hiyo kugawiwa pande mbili nyingine ikiitwa East Germany].

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Germany XI: Ter Stegen, Howedes, Mustafi, Hummels, Kimmich, Kroos, Khedira, Can, Sane, Weigl, Podolski, Muller

England XI: Hart, Walker, Cahill, Stones, Bertrand, Dier, Alli, Lallana, Oxlade-Chamberlain, Sterling, Rashford

KIMATAIFA – Kirafiki:

Jumatano Machi 22

**Saa za Bongo

1900 Cyprus v Kazakhstan

2000 Czech Rep v Lithuania

2245 Scotland v Canada

2245 Germany v England