EFL CUP - NUSU FAINALI: JUMANNE KUANZA OLD TRAFFORD MAN UNITED v HULL CITY!

EFL CUP
Nusu Fainali
**Saa za Bongo
Jumanne Januari 10
2300 Manchester United v Hull City
Jumatano Januari 11
2245 Southampton V Liverpool
=============================
IMG-20170109-WA0000NUSU FAINALI za Kombe la Ligi hukoEngland ambalo sasa huitwa EFL CUP (English Football League Cup) zitaanza Jumanne Januari 10 huko Old Trafford kwa Manchester
 United kucheza na Hull City.
Siku ya Pili, Jumatano Januari 11, itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Kwenye Mechi ya Old Trafford, Meneja wa Man United Jose Mourinho amedokeza atabadili Kikosi chake toka kile kilichoichapa Reading 4-0 Jumamosi katika Raundi ya 3 ya FA CUP.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alieleza: "Jumamosi tumecheza na Wachezaji freshi. Ila sitaki ieleweke tuna Timu ya Kwanza au ya Pili! Wachezaji ambao hawakucheza Mechi hii watacheza na Hull..hivyo ni rahisi kujua Zlatan, Pogba, Herrera, Valencia watarudi Mechi na Hull."
+++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
+++++++++++++++++
Hull City, chini ya Meneja Mpya Marco Silva kutoka Ureno alietwaa mikoba ya Mike Phelan alietimuliwa Wiki iliyopita, itatinga Old Trafford ikiwa na Difensi ya kuungaunga kutokana na Majeruhi kadhaa.
Sentahafu wao Michael Dawson aliumia na kutolewa Kipindi cha Pili Juzi kwenye FA CUP walipoifunga Swansea City na nafasi hiyo kushikwa na Kiungo Tom Huddlestone alishirikiana na Kiungo mwingine Jake Livermore.
Beki mwingine Majeruhi wa Hull ni Curtis Davis na hivyo kuwaacha Hull kutumia Viungo Watatu kwenye Nafasi 4 za Difensi yao.
Nafasi ya Fulbeki wa Kulia imelazimika kuzibwa na David Meyler baada kumpoteza Ahmed Elmohamady ambae ameenda Egypt kujiunga na Timu ya Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoanza huko Gabon Januari 14.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
**Saa za Bongo
Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton
Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United