EFL CUP – NUSU FAINALI: MATA. FELLAINI WAIWEKA MAN UNITED GUU MOJA FAINALI!

>LEO ‘WATAKATIFU’ NA LIVERPOOL KWA MTAKATIFU MARIA!

EFL-CUP-2016-17EFL CUP

Nusu Fainali

Ratiba/Matokeo:

Jumanne Januari 10

Manchester United 2 Hull City 0

Jumatano Januari 11

**Saa za Bongo

2245 Southampton V Liverpool

++++++++++++++++++++++++

Manchester United, ikiongozwa na MenejaJose Mourinho, wamepiga hatua kubwa kuelekea kutwaa Taji kubwa la pili Msimu huu baada ya Jana huko kwao Old Trafford kuichapa Hull City 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England.

Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.

Bao za Man United, waliochezesha karibu Kikosi chao chote, zilifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini alieanzia Benchi.

Bao la Mata lilifungwa Dakika ya 56 alipounganisha Kichwa cha Henrikh Mkhitaryan na la pili Dakika ya 87 kupitia Fellaini alieunganisha Krosi ya Matteo Darmian.

Hull City na Man United zitarudiana huko KCOM Stadium hapo Januari 28.

+++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.

-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.

+++++++++++++++++++++++++

Leo Jumatano Januari 11 itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.

Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.

EFL CUP

Nusu Fainali

MARUDIANO

**Saa za Bongo

**Kwenye Mabano Mabao Mechi ya Kwanza

Jumatano Januari 25

2300 Liverpool v Southampton

Alhamisi Januari 26

2245 Hull City v Manchester United [0-2]