COPA DEL REY: MESSI, NEYMAR, ALCACER WAIPA KOMBE BARCA!

COPAREY17BARCELONA Jana waliipiga Alaves Bao 3-1 kwenye Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey na kujipa ahueni baada Wiki iliyopita kushindwa kuutetea Ubingwa wao wa La Liga ulioenda kwa Mahasimu wao Real Madrid.
Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Barca kutwaa Kombe hili.
Fainali hii ilichezwa huko Vicente Calderon Jijini Madrid na ndio Mechi ya mwisho kabisa kwa Kocha wa Barca Luis Enrique ambae anaondoka Klabuni hapo.
Bao zote za Mechi hiyo zilifungwa Kipindi cha Kwanza.
Barca walitangulia kufunga Dakika ya 30 kupitia Lionel Messi na Alaves kusawazisha kwa Frikiki ya Theo Hernandez Dakika ya 33.
Barca walipiga Bao 2 za chapchap Dakika za 45 na 48 kupitia Neymar na Alcarer na kwenda Haftaimu 3-1 mbele.

 
 

MESSI: RUFAA YATUPWA, JELA MIEZI 21 PALE PALE!

BARCA-MESSI-SITADHABU ya Kifungo cha Jela cha Miezi 21 alichoshushiwa Mchezaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi itabaki pale pale baada kuthibitishwa na Mahakama ya Rufaa ya Spain.
Hata hivyo, huko Spain, Vifungo vya chini ya Miezi 24 si lazima ukae lupango na badala yake unaweza kupewa Kifungo cha Nje.
Mwaka Jana, Messi na Baba yake Mzazi aitwae Jorge walihukumiwa Jela kwa Kosa la Ukwepaji Kodi wa Euro Milioni 4.1.
Kosa hilo linahusiana na kuanzisha Kampuni feki huko Belize na Uruguay kusimamia Mauzo ya Hatimiliki za Picha na Matangazo yanayomhusu Messi ili kukwepa kulipa Kodi huko Spain.
Kifungo cha Babae Messi, ambae alihukumiwa Miezi 24 Jela, kilipunguzwa hadi Miezi 15 baada ya kulipa Kodi zilizokwepwa.
Kesi hii sasa imerejeshwa Mahajama ya Mjini Barcelona ili kuamua aina ya Adhabu ikiwa ni Jela au Kifungo cha Nje.

REAL MADRID YAMSAINI KINDA MBRAZIL MIAKA16 KWA £39.6 MILIONI!

VINICIUSMABINGWA WAPYA wa Spain Real Madrid wamemsaini Vinícius Júnior kutoka Flamengo ya Brazil kwa Dau la Pauni Milioni 39.6.
Tineja huyo amekichezea Kikosi cha Kwanza cha Flamengo Mechi 1 tu.
Inadaiwa Klabu za Barcelona na Manchester United zilitoa Ofa za Euro Milioni 30 lakini ile ya Euro Milioni 46 ya Real ndio imewini.
Vinícius Júnior alisaini Mkataba Mpya na Flamengo Wiki iliyopita na ndani yake kubadilishwa Kipengele cha Kuuzwa kwake wakati Mkataba ukiwa hai kutoka Euro Milioni 30 hadi 46 ambazo ndizo Real wamelipa.
Dili hii imemfanya Kinda huyu kuwa Mchezaji wa Bei mbaya wa Pili kununuliwa katika Historia ya Brazil baada Neymar kununuliwa na Barcelona kutoka Santos Mwaka 2013 kwa Dau la Euro Milioni 86.
Mara baada Dili ya Kijana huyu kukamilika, Real imetangaza kuwa wataanza kummiliki Mchezaji huyu kuanzia Julai 2018 akitimiza Miaka 18 lakini atabaki Flamengo hadi Julai 2019.
Vinicius ameichezea Timu ya Taifa ya Brazil ya U-17 mara 22 akipachika Bao 19.
Kwenye Ubingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini w U-17, Vinicius ndie aliibuka Mchezaji Bora na Mfungaji Bora akipiga Bao 7.

LA LIGA: REAL MADRID MABINGWA, RONALDO AWASETIA UBINGWA WA KWANZA TANGU WA JOSE MOURINHO 2012!!

>ZAMA ZA BARCA KWISHNEI!

JANA, La Liga, ilifikia tamati na Real Madrid kuutwaa Ubingwa baada ya kuichapa Ugenini Malaga 2-0.

Huo na Ubingwa wa Kwanza wa La Liga kwa Real tangu wautwae Mwaka 2012 chini ya Meneja wa sasa wa Manchester United Jose Mourinho.

Pia Real sasa wako njiani kutwaa Dabo, Ubingwa wa Spain na UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa mara ya kwanza katika Miaka 59.

Juni 3, Real wapo huko Cardiff, Wales kucheza na Juventus katika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Jana, Real walikwenda mbele 1-0 Dakika ya Pili tu baada Krosi tamu ya Isco kumkuta Cristiano Ronaldo aliefunga.

Dakika ya 55 Real walikwenda 2-0 mbele kufuatia Kona ya Toni Kroos kuunganishwa na Sergio Ramos na Kipa Kameni kuokoa na Mpira kumgonga Varane na kudondokea kwa Karim Benzema aliekwamisha Wavuni.

Mara baada ya Mechi hiyo kwisha Jiji la Madrid huko Spain lilizima kwa Shangwe na Mashabiki wa Real kusongana katikati ya Mji kwenye Chemchem ya Cebeles kusheherekea kama ilivyo desturi yao huku Uwanja wa Malaga ukiwa hoihoi.

VIKOSI:

MALAGA: Kameni, Torres, Hernandez, Mikel, Ricca, Camacho, Keko, Recio, Fornals, Jony, Sandro.

REAL MADRID: Navas, Danilo, Varane, Ramos, Marcelo, Casemiro, Modric, Kroos, Isco, Ronaldo, Benzema.

BARCA 4 EIBAR 2

Barcelona Jana walivuliwa Ubingwa na kutwaa Nafasi ya Pili ya La Liga na kuwa Pointi 3 nyuma ya Mabingwa Real Madrid baada ya wao kutoka nyuma 2-0 na kuilaza Eibar 4-2.

Eibar walifunga Bao zao Dakika 7 na 61 kupitia Takashi Inui na Barca kujibu Dakika za 63, 73, 75 na 92 Wafungaji wakiwa Junca, aliejifunga mwenyewe, Luis Suarez na 2 za Lionel Messi ambae pia alikosa Penati na ufunga nyingine.

Bao za Messi zimemfanya azoe Buti ya Dhahabu ya La Liga kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2012/13.

VIKOSI:

BARCELONA: Ter Stegen, Roberto, Umtiti, Marlon, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.

EIBAR: Yoel, Capa, Lejuene, Arbilla, Junca, Pena, Dani Garcia, Escalante, Inui, Enrich, Kike.

LA LIGA 

Matokeo:

Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
Granada 1 Espanyol 2 

Jumamosi Mei 20
Deportivo 3 Las Palmas 0 
Sporting Gijon 2 Real Betis 2 
Leganes 1 Alaves 1 

Sevilla 5 Osasuna 0
Jumapili Mei 21
Atletico Madrid 3 Athletic Club 1 
Celta Vigo 2 Real Sociedad 2
Valencia 1 Villarreal 4
Barcelona 4 Eibar 2 
Malaga 0 Real Madrid 2 

LA LIGA: REAL NA UBINGWA JUMAPILI HUKO MALAGA, YAKUMBUSHWA KILIO CHA TENERIFE, BARCA WAHOFU MALAGA KULA NJAMA!

>PATA UNDANI!

REAL-MABINGWA WARAJIWAJUMAPILI, La Liga, Ligi kubwa huko Nchini Spain, inafunga Pazia lake kwa Msimu wa 2016/17 na Bingwa atakuwa Real Madrid au Barcelona.

Real wapo Pointi 3 mbele ya Barcelona na Jumapili wanamaliza Ugenini kwa kucheza na Malaga wakati  Barcelona wapo Nyumbani kupambana na Eibar.

Real wanahitaji Pointi 1 toka Timu ambayo waliifunga 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya La Liga Msimu huu ili watwae Ubingwa wao wa kwanza wa La Liga tangu 2012.

Lakini Wachambuzi wengi huko Spain wamekumbusha nini kiliwatokea Real Mwaka 1993.

Wakihitaji Pointi 1 tu kuwa Mabingwa katika Mechi ya Mwisho ya Msimu, Real waliruka kwenda Visiwani Tenerife na kufungwa na Ubingwa ukaenda kwa Barcelona walioshinda Mechi yao.

Siku hiyo huko Tenerife mmoja wa Wachezaji wa Real Madrid alikuwa Kiungo wao Michel Gonzalez ambae alinaswa kwenye Picha akiwa na huzuni kubwa huku akifarijiwa Uwanjani na Mchezaji wa Tenerife Quique Estebaranz.

Sasa Michel Gonzalez, ambae alianzia utotoni kuichezea Real na kupanda hadi Timu ya Kwanza alikokaa kwa Miaka 14, ndie Meneja wa Malaga ambao wanaweza kuisimamisha Real kutwaa Ubingwa.

Hii Leo huko Spain, Michel Gonzalez amebatizwa Jina la ‘Jaji wa Ligi’ kutokana na hii Mechi na Real itakayoamua Bingwa.

Huko Spain zishazagaa Stori za Njama za kuipa Real Ubingwa na baadhi kudai Michel Gonzalez anataka Real ishinde.

Pia, Rais wa Malaga, anadaiwa kuwaita Barcelona ‘takataka’ na kusema ‘hawatasikia hata harufu ya Ubingwa’!

Lakini pia upo ukweli kwamba Malaga ina Wachezaji Watano wenye asili ya Real na pia Mkataba wa Kiungo wa Real, Isco, kuuzwa kutoka Malaga kwenda Real una kipengele cha kuilipa Malaga Bonasi ya Euro Milioni 3 endapo Real watatwaa Ubingwa.

Mambo hayo yamelifanya Gazeti moja la huko Mjini Barcelona liandike Bango kubwa: ‘MALAGA INANUKIA NYEUPE!” ikimaanisha Malaga ni Real Madrid.

Hilo pengine ni chuki hasa wakikumbuka Msimu huu Malaga iliiwasha Barcelona 2-0 ndani ya Nou Camp.

Kwa upande wa Soka, hiyo Jumapili Barcelona inabidi kwanza waifunge Eibar na ndio waombe Real iteleze huko Malaga.

Mvuto wa Mechi hii ya Barcelona na Eibar ni kuwa Mtoto wa Kocha wa Malaga, Michel Gonzalez, anaeitwa Adrian ni Mchezaji wa Eibar.

Ukiitazama Real kufungwa na Malaga, ambayo ukweli ipo salama La Liga, na pia hivi sasa mwendo wake ni mbendembende, ni ndoto na hasa ukizingatia Real imefungwa Mechi 3 tu Msimu mzima.

Katika Mechi 3 zilizopita, Real imebonda Bao 4 kila Mechi huku Nyota wao, Cristiano Ronaldo, akionekana yuko fiti na moto baada ya kukosa Mechi 14 Msimu huu kutokana na maumivu.

Katika Mechi 8 zilizopita, Ronaldo amepiga Bao 13.

LA LIGA 

Ratiba/Matokeo:

Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
Granada 1 Espanyol 2 

Jumamosi Mei 20
18:00 Deportivo v Las Palmas 
18:00 Sporting Gijon v Real Betis 
18:00 Leganes v Alaves 

Jumapili Mei 21
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club 
17:45 Celta Vigo v Real Sociedad 
17:45 Sevilla v Osasuna 
17:45 Valencia v Villarreal 
21:00 Barcelona v Eibar 
21:00 Malaga v Real Madrid