WABABE SPAIN REAL, BARCA KUANZA 2017 KWA COPA DEL REY JUMATANO NA ALHAMISI!

LALIGA-2016-17SOKA la Spain litarejea dimbani Mwaka huu Mpya kuanzia Leo Usiku kwa Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, lakini Vigogo wa huko, Real Madrid na FC Barcelona, wao wataonekana Jumatano na Alhamisi.

Jumatano, Real wapo kwao Santiago Bernabeu kucheza na Sevilla na Alhamisi ni FC Barcelona Ugenini na Athletic Bilbao.

Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni Wiki ijayo.

La Liga itaanza rasmi Mwaka 2017 hapo Ijumaa na Real, ambao ndio Vinara, kuwa dimbani kwao Bernabeu Jumamosi na Granada wakati Mabingwa Watetezi, Barca, ambao wako Nafasi ya Pili, watacheza Jumapili Ugenini na Villareal.

COPA DEL REY

Ratiba

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Januari 3

2100 Osasuna v SD Eibar  

2100 Valencia C.F v Celta de Vigo

2315  Deportivo La Coruna v Deportivo Alaves

2315  Las Palmas v Atletico de Madrid  

Jumatano Januari 4

2100  Real Sociedad v Villarreal CF       

2100  Alcorcon v Cordoba CF     

2315  Real Madrid CF v Sevilla FC

Alhamisi Januari 5

2315  Athletic de Bilbao v FC Barcelona