COPA DEL REY: REAL, BILA RONALDO, YATIKISA!!

REAL-SEVILLASOKA la Spain limarejea dimbani Mwaka huu Mpya kwa Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, na Real Madrid Jana kuanza kwa kishindo huko Santiago Bernabeu kwa kuicharaza Sevilla 3-0 wakicheza bila ya Staa wao Cristiano Ronaldo ambae ndie Mchezaji Bora Duniani.

Real, ambao wameshinda Mechi 29 kati ya 38 zilizopita bila kufungwa na wamebakisha Mechi 1 tu kuifikia Rekodi Bora ya Klabu za La Liga ya kucheza Mechi nyingi bila kufungwa.

Bao za Real hapo Jana zilifungwa na James Rodriguez, Bao 2 moja ikiwa ni Penati, na jingine Mfungaji alikuwa Raphael Varne.

Timu hizi zitarudiana tena huko Seville hapo Januari 12 na Real wataanza kipindi cha kucheza Mechi 21 katika Wiki 11.

Leo Alhamisi Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey FC Barcelona wapo Ugenini kuchezana Athletic Bilbao.

La Liga itaanza rasmi Mwaka 2017 hapo Ijumaa na Real, ambao ndio Vinara, kuwa dimbani kwao Bernabeu Jumamosi na Granada wakati Mabingwa Watetezi, Barca, ambao wako Nafasi ya Pili, watacheza Jumapili Ugenini na Villareal.

COPA DEL REY

Ratiba/Matokeo:

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Januari 3

Osasuna 0 SD Eibar 3       

Valencia C.F 1 Celta de Vigo 4     

Deportivo La Coruna 2 Deportivo Alaves 2       

Las Palmas 0 Atletico de Madrid 2

Jumatano Januari 4

Real Sociedad 3 Villarreal CF 1    

Alcorcon 0 Cordoba CF 0  

Real Madrid CF 3 Sevilla FC 0      

Alhamisi Januari 5

2315  Athletic de Bilbao v FC Barcelona 

 

NEYMAR: ‘SINA MCHECHETO NA Ballon d'Or'

STAA wa Barcelona kutoka Brazil, Neymar, amesema kutwaa Tuzo ya Ballon d'Or ni moja ya malengo yake lakini hatapoteza usingizi ikiwa hatatwaa Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka.

Akiongea kwenye Mahojiano na Mtandao rasmi wa La Liga ya Spain, Neymar, ambae hakuwemo kwenye 3 Bora ya waliowania Tuzo hii kwa Mwaka huu, amesema: “Kama sitatwaa Ballon d'or, ni sawa tu. Sichezi Soka kushinda Ballon d'or, nacheza Soka kuwa na furaha kwa sababu napenda Soka, nataka nicheze Soka. Kwa bahati mbaya Mtu mmoja tu hutwaa Tuzo hiyo!”

Aliongeza: “Ni wazi, ni moja ya malengo yangu kushinda Ballon d'or, lakini sitakufa kama sikutwaa!”

Tuzo ya Ballon d'or imekuwa ikibadilishana kati ya Staa wa Real Madrid kutoka Ureno, Cristiano Ronaldo, na Mchezaji wa Barcelona anaetoka Argentina, Lionel Messi, kwa Miaka 9 iliyopita tangu Mbrazil Kaka alipoitwaa Mwaka 2007.

Mwaka Jana, 2015, Neymar alifika 3 Bora ya Ballon d'or, na Messi kuitwaa Tuzo hiyo kwa mara ya 5 na Mwaka huu, Ronaldo kuizoa.

Tangu ajiunge na Barcelona Mwaka 2013 akitokea Klabu ya Brazil Santos, Neymar ametwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Makombe mengine huko Spain mara 2 pamoja na Super Cup ya Spain, UEFA CHAMPIONZ LIGI na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu.

LA LIGA

Ratiba

Ijumaa Januari 6

RCD Espanyol v Deportivo La Coruna

Jumamosi Januari 7

Real Madrid CF v Granada CF

SD Eibar v Atletico de Madrid

Celta de Vigo v Malaga CF

Real Sociedad v Sevilla FC

Jumapili Januari 8

Athletic de Bilbao v Deportivo Alaves

Real Betis v CD Leganes

Las Palmas v Sporting Gijon

Villarreal CF v FC Barcelona

Jumatatu Januari 9

Osasuna v Valencia C.F