COPA DEL REY: BARCELONA YACHAPWA NA MTU 9 BILBAO!!

BILBAO-BARCAMABINGWA Watetezi wa Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, FC Barcelona, Jana wameanza vibaya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kuchapwa na Mtu 9 Athletic Bilbao 2-1.

Bilbao, wakicheza kwao, walifunga Bao zao 2 ndani ya Dakika 3 za Kipindi cha Kwanza, Dakika za 25 na 28, kupitia Aritz Aduriz na Inaki Williams.

Lionel Messi akaipa Barca Bao lao moja kwa Frikiki ya Dakika ya 52 na baadae kukosa Goli katika Dakika za Majeruhi alipogonga Posti huku Bilbao wakiwa Mtu 9 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Raúl García, Dakika ya 74, na Iturraspe Derteano, Dakika ya 80, wote wakiwa wamepewa Kadi za Njano 2 kila mmoja.

La Liga itaanza rasmi Mwaka 2017 Leo Ijumaa na Real, ambao ndio Vinara, kuwa dimbani kwao Bernabeu Jumamosi na Granada wakati Mabingwa Watetezi, Barca, ambao wako Nafasi ya Pili, watacheza Jumapili Ugenini na Villareal.

COPA DEL REY

Ratiba/Matokeo:

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Januari 3

Osasuna 0 SD Eibar 3       

Valencia C.F 1 Celta de Vigo 4     

Deportivo La Coruna 2 Deportivo Alaves 2       

Las Palmas 0 Atletico de Madrid 2

Jumatano Januari 4

Real Sociedad 3 Villarreal CF 1    

Alcorcon 0 Cordoba CF 0  

Real Madrid CF 3 Sevilla FC 0      

Alhamisi Januari 5

Athletic de Bilbao 2 FC Barcelona 1