LA LIGA: MECHI ZA KWANZA MWAKA MPYA 2017, REAL JUMAMOSI BERNABEU NA GRANADA, BARCA UGENINI JUMAPILI VILLAREAL!

LALIGA-2016-17LA LIGA, Ligi ya Nchini Spain, inarejea tena kwa mara ya kwanza kwa Mwaka huu mpya 2017 Wikiendi hii kuanzia Ijumaa.

Vinara wa La Liga Real Madrid watakuwa kwao Santiago Bernabeu kucheza na Granada huku Mabingwa Watetezi Barcelona watakuwa Ugenini kucheza Mechi inayoitwa ‘Ganda la Ndizi’ dhidi ya Villareal hapo Jumapili.LALIGA-JAN06

Mechi hizi zinakuja baada Kati Wiki Timu hizo kuanza 2017 kwa Mechi za Raundi ya 3 za Copa del Rey ambapo Real, wakicheza bila ya Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo, kuichapa Sevilla 3-0 na Barca, wakiwa nae Staa wao mkubwa Lionel Mess, kufungwa 2-1 na Athletic de Bilbao.

Ukiziondoa Real na Valencia, ambao wamecheza Mechi 15, Timu zote zilizobakia zimecheza Mechi 16 na Real ndio Vinara wakiwa na Pointi 37 wakifuata Barca wenye 34 na kisha Sevilla wenye 33.

LA LIGA

Ratiba

**Saa za Bongo

Ijumaa Januari 6

2145 RCD Espanyol v Deportivo La Coruna

Jumamosi Januari 7

1500 Real Madrid CF v Granada CF

1815 SD Eibar v Atletico de Madrid

2030 Celta de Vigo v Malaga CF

2245 Real Sociedad v Sevilla FC

Jumapili Januari 8

1400 Athletic de Bilbao v Deportivo Alaves

1815 Real Betis v CD Leganes

2030 Las Palmas v Sporting Gijon

2245 Villarreal CF v FC Barcelona

Jumatatu Januari 9

2245 Osasuna v Valencia C.F