REAL WAANZA MWAKA MPYA LA LIGA KWA KISHINDO, WAISHIKA REKODI YA BARCA!

LALIGA-2016-17-2Real Madrid wameikamata Rekodi ya Barcelona ya kutofungwa katika Mechi 39 za Mashindano yote baada ya Jana kuitandika Granada 5-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2017 ya La Liga iliyochezwa Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain.
Ushindi huo umeifanya Real izidi kuongoza La Liga sasa ikiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili FC Barcelona ambao ndio Mabingwa Watetezi.
Hiyo Jana, Bao za Real zilipachikwa na Isco, Dakika za 12 na 31, Karim Benzema, 20, Cristiano Ronaldo, 27 na Casemiro, 58.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Januari 6
RCD Espanyol 1 Deportivo La Coruna 1
Jumamosi Januari 7
Real Madrid CF 5 Granada CF 0
SD Eibar 0 Atletico de Madrid 2
Real Sociedad 0 Sevilla FC 4
Las Palmas 1 Sporting Gijon 0
Jumapili Januari 8
1400 Athletic de Bilbao v Deportivo Alaves
1815 Real Betis v CD Leganes
2030 Celta de Vigo  Malaga CF
2245 Villarreal CF v FC Barcelona
Jumatatu Januari 9
2245 Osasuna v Valencia C.F