COPA DEL REY: SUAREZ, NEYMAR, MESSI WAIPENYEZA BARCA ROBO FAINALI!!

BARCA-TRIO-MSN 1BAO za Suarez, Neymar na Messi zimewapeleka Mabingwa Watetezi FC Barcelona Robo Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, walipoifunga Athletic Bilbao 3-1 huko Nou Camp hapo Jana.

Wakiwa wamefungwa 2-1 katika Mechi ya Kwanza, Barca walitangulia kufunga Dakika ya 36 kwa Bao la Luis Suarez likiwa Bao lake la 100 katika Mechi 120 za Barca.

Neymar aliongeza Bao la Pili Dakika ya 47 na Bilbao kupiga Bao lao moja Dakika ya 51 kupitia Saborit na kufanya Gemu iwe Sare 3-3 kwa Mechi 2 lakini Messi akapiga Bao la 3 Dakika ya 70 na kuwapa Barca ushindi wa 3-1 na 4-3 kwa Mechi Mbili.

COPA DEL REY

Ratiba/Matokeo:

Raundi ya Mtoano ya Timu 16 – Marudiano

Jumanne Januari 10

Atletico de Madrid 2 Las Palmas 3 [Mechi Mbili: 4-3]

Jumatano Januari 11

Deportivo Alaves v Deportivo La Coruna [2-2]  

Villarreal CF 1 Real Sociedad 1 [2-4]     

Cordoba CF 1 Alcorcon 2 [1-2]    

FC Barcelona 3 Athletic de Bilbao 1 [4-3]

Alhamisi Januari 12 

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza 

21:00 Celta de Vigo v Valencia C.F [4-1]         

21:00 SD Eibar v Osasuna [3-0] 

23:15 Sevilla FC v Real Madrid CF [0-3]