ICC SINGAPORE: BAYERN YAICHARAZA CHELSEA 3, MORATA NDANI KWA MARA YA KWANZA!

BAYERN CHELSEABAO 2 za Thomas Muller zimeisaidia Bayern Munich kuifunga Chelsea 3-2 kwenye Mechi ya International Champions Cup iliyochezwa Leo huko National Stadium, Singapore huku macho ya wengi yakitaka kumuona Mchezaji mpya Alvaro Morata wa Chelsea.
Rafinha ndie alieipa Bayern Bao la kuongoza Dakika ya 6 tu kwa Shuti la mbali na Dakika 6 baadae Muller akaiweka Bayern 2-0 mbele.
Alikuwa tena Muller alieipa Bayern Bao la 3 Dakika ya 27 kwa mzinga mkali uliomwacha Kipa Thibaut Courtois taabani.
Marcos Alonsor akaipa Chelsea Bao Dakika chache kabla Haftaimu na kufanya Gemu iwe Bayern 3 Chelsea 1 wakati wa Mapumziko.
Meneja Antonio Conte alimuingiza Alvaro Morata katika Dakika ya 63 kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Chelsea tangu ahamie hapo kutoka Real Wiki iliyopita.
Lakini ni Michy Batshuayi alieipigia Chelsea Bao la Pili Dakika ya 85.
Mechi hii iliisha Bayern 3 Chelsea 2.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Bayern Munich (Mfumo 4-2-3-1): Starke (Fruchtl 46), Rafinha (Pantovic 63), Hummels, Martinez, Friedl; Sanches, Tolisso ( Gotze 63),  James, Muller (Wintzheimer 81), Ribery (Dorsch 81), Lewandowski (Coman 46)
Bayern Munich substitutes: Gotze, Ulreich, Alaba, Coman, Dorsch, Fruchtl, Wintzheimer, Pantovic, Hofmann.
Chelsea (Mfumo 3-4-3): Courtois (Eduardo 76), Azpilicueta, Christensen (David Luiz 63), Cahill; Moses, Kante, Fabregas (Baker 86), Alonso (Tomori 86); Willian, Batshuayi (Pasalic 86) Boga (  Morata 63)
Chelsea substitutes: Caballero, Morata, Remy, Luiz, Tomori, Kalas, Bulka, Baker, Clarke-Salter, Scott, Eduardo, Pasalic.
REFA: Taqi

Chelsea

22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing [3-0]

25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup) (2-3)

29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)

JUMANNE CHELSEA v BAYERN HUKO SINGAPORE, MORATA NDANI CHELSEA, JAMES RODRIGUEZ NDANI BAYERN!

CHELSEA PREJUMANNE, Saa 8 Dakika 35 Mchana, Saa za Bongo, kipo kivumbi cha kugombea International Champions Cup, ICC, huko National Stadium, Singapore kati ya Mabingwa wa England Chelsea na Mabingwa wa Germany Bayern Munich.

Kila Timu inatarajiwa kuwatumia Mastaa wao wapya wote kutoka kwa Mabingwa wa Spain na Ulaya Real Madrid kwa Chelsea kumchezesha Alvaro Morata na Bayern kumtumia James Rodriguez.

Chelsea Juzi iliicharaza Arsenal 3-0 huko Bird’s Nest Stadium, Beijing katika Mechi ya Kirafiki wakati Bayern ikitoka Sare 1-1 na Arsenal na kisha kubwagwa kwa Mikwaju ya Penati na Mechi iliyofuata kutandikwa 4-0 na AC Milan.

Baada Mechi hii na Bayern, Jumatano Bayern wataivaa Inter Milan na Jumamosi Chelsea watacheza na Inter Milan katika Mechi nyingine za ICC zote zikiwa huko huko Singapore.

Bayern wapo chini ya Meneja Carlo Ancelotti ambae aliwahi kwa Misimu Miwili kuwa Meneja wa Chelsea na Antonio Conte yupo Chelsea kwa Msimu wake wa Pili baada Msimu uliopita kuwapa Ubingwa wa England.

ICC SINGAPORE

Chelsea

22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing [3-0]

25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)

ARSENE WENGER ANG’ANG’ANIA ALEXIS SANCHEZ HAUZWI ILA TIMU ZINAMRUBUNI!

ARSENAL SANCHEZ HATIMAHUKU kukiwa na ripoti thabiti kuwa Klabu Tajiri Paris Saint-Germain wako tayari kurejea na Ofa kubwa ya kumnunua Sanchez, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameng’ang’ania Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Chile hauzwi kwa Bei yeyote na wao hawahitaji Fedha za Mauzo kwa Mchezaji wao yeyote.

Licha Sanchez kugoma kusaini Mkataba Mpya huku akiingia Mwaka wa Mwisho wa Mkataba wake na Arsenal, Klabu hiyo haitaki kumuuza sasa ili waambulie Dau nono na hivyo kuleta hatari Mwakani akaondoka bila kuambua hata Senti.

Mbali ya PSG, pia Manchester City nao wameripotiwa kujiingiza kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua Mchezaji huyo mwenye Umri wa Miaka 28.

Akiongea kuhusu Sanchez, Wenger amesisitiza: “Nilishaamua kitambo. Nimeelezea mara kadhaa, atabakia Arsenal. Sanchez amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na hatuhitaji kuzalisha Fedha. Atabakia hapa Mwaka Mmoja zaidi na baada ya hapo tunaelewa!”

Aliongeza: “Tupo hali njema Kifedha hivyo tutabakisha Wachezaji wetu wote wazuri. Je ameomba kuhama? Hapana!”

Sanchez anatarajiwa kurejea Emirates Jumatatu ijayo baada ya kupewa likizo ndefu kutokana na kuiwakilisha Nchi yake Chile kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Russia mapema Mwezi huu.

Alipoulizwa ikiwa anahisi kuwa zipo Klabu zinamrubuni Sanchez aihame Arsenal, Wenger alijibu: “Hivi unafikiriaje? Ukiwa na Wachezaji bora hilo halizuiliki. Utazuiaje Wakala kuongea na Mkurugenzi wa Klabu nyingine au Mchezaji mwenyewe kukutana na Watu wa Klabu nyingine? Hili linatokea kila Siku. Halijapatiwa ufumbuzi!”

Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

Arsenal

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup [1-1, Penati 3-2]

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing) [0-3]

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)

 

MINOTI YA PSG YAMLENGA SANCHEZ LICHA WENGER KUPIGA YOWE HAUZWI!!!

LICHA Meneja wa Arsenal kudai Alexis Sanchez hauzwi, Klabu Tajiri Paris Saint-Germain imemweka Fowadi huyo kutoka Chile kama Mlengwa wao Nambari Wani katika kipindi hiki cha Uhamisho.
ARSENAL SANCHEZ HATIMAHivi sasa Sanchez ameanza Mwaka wa mwisho wa Mkataba wake na Arsenal huku akigomea kusaini Mkataba mpya na pia kudai Msimu ujao mpya anataka kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI wakati Arsenal wakishiriki UEFA EUROPA LIGI.
Akiongea huko China ambako wako Ziarani, Wenger amesisitiza: "Uamuzi ni kutomuuza!"
Alipoulizwa kuhusu matakwa ya Sanchez kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Mashindano ambayo Arsenal hawamo, Wenger alijibu: "Siweki umuhimu kwa vitu vinavyotafsiriwa. Mahojiano yote ya Sanchez nnayo na hakumaanisha hilo!"
Aliongeza: "Mkazo mkubwa kwetu ni Ligi Kuu na kwetu Ligi Kuu ni muhimu kupita Championz Ligi!"
Wenger alihitimisha: "Tumecheza Championz Ligi kwa Miaka 20 na hiyo ni
Miaka 17 kabla Sanchez kuja na Miaka Mitatu tukiwa nae, hivyo yeye ataturudisha huko Championz Ligi."
Mwanzoni iliaminika Sanchez anataka kutua Man City lakini sasa ikiwa kweli PSG wanamwania basi itakuwa ngumu kwa Arsenal kumzuia kuhama hasa kwa vile Klabu hiyo Tajiri ina Bajeti ya zaidi ya Pauni Milioni 200 kununua Wachezaji Wapya katika Kipindi hiki.

DIEGO COSTA NA NEMANJA MATIC WAACHWA ZIARA YA CHELSEA YA CHINA!

>KUZIKOSA MECHI ZA ZIARA DHIDI YA ARSENAL, BAYERN NA INTER!

CHELSEA COSTA MATICDiego Costa na Nemanja Matic hawamo kwenye Kikosi cha Chelsea ambacho Jumatatu kitaruka kwenda China kuanza Ziara yao ya Matayarisho ya Msimu Mpya huku kukiwa na ripoti kuwa Wachezaji hao watawahama Mabingwa hao wa England.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amewajulisha Wachezaji hao Wawili kuwa hawamo kwenye Msafara.

Straika Diego Costa, Mchezaji wa Kimataifa wa Spain mwenye Umri wa Miaka 28, anataka kurejea Klabu aliyotokea Atletico Madrid licha ya kuwa hataweza kusajiliwa na kucheza hadi Januari Mwakani kwa vile Klabu hiyo inatumikia Kifungo cha FIFA cha Kutosajili Wachezaji Wapya kwa kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi.

Nae Nemanja Matic, mwenye Miaka 28, anatakiwa na Man United na Klabu kadhaa za Italy huku mwenyewe akitaka kuhama hasa baada ya Chelsea kumsaini Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko ambae anatarajiwa kumbadili Matic kwenye Kikosi cha Kwanza.

Matic alirejeshwa Chelsea kwa mara ya pili Mwaka 2014 na Jose Mourinho wakati alipokuwa Meneja huko na sasa Mchezaji huyo anatamani sana kuungana tena na Mourinho huko Man United.

Kwenye Ziara yao huko China, Chelsea wataanza kucheza Julai 22 na Arsenal na kisha kuruka kwenda Singapore kucheza na Bayern Munich na Inter Milan

Chelsea - Mechi za Ziara:

22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing

25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)