SERIE A: GONZALO HIGUAIN AIPAISHA JUVE POINTI 7 KILELENI!

HIGUAIN-BAO-ROMABAO la Dakika ya 14 la juhudi binafsi za Gonzalo Higuain limewapa ushindi Juventus wa Bao 1-0 dhidi ya AS Roma na kufungua pengo la Pointi 7 kwa Juve kuongoza Serie A mbele ya Timu ya Pili AS Roma.

Kwa Juve, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Serie kwa Miaka Minne iliyopita, huu ulikuwa ushindi wao wa 25 mfululizo wa Nyumbani kwenye Serie A na kuifikia Rekodi yao SERIEA-DES18waliyoiweka kati ya Agosti 2013 na Desemba 2014.

Hicho kilikuwa kipigo cha 6 mfululizo kwa AS Roma ndani ya Juventus Stadium Jijini Turin.

Juve waliingia kwenye Mechi hii bila ya Leonardo Bonucci na Dani Alves wakati AS Roma wakiwakosa Mohamed Salah na Bruno Peres.

VIKOSI:

Juventus: Buffon; Lichtsteiner (Barzagli 68), Rugani, Chiellini, Alex Sandro; Khedira, Marchisio, Sturaro; Pjanic (Cuadrado 51); Mandzukic, Higuain (Dybala 82)

Roma: Szczesny; Rudiger, Manolas (Bruno Peres 85), Fazio, Emerson Palmieri; De Rossi (El Shaarawy 72), Strootman; Gerson (Salah 46), Nainggolan, Perotti; Dzeko

REFA: Orsato

SERIE A

Matokeo

Jumamosi Desemba 17

Empoli 2 Cagliari 0

Juventus 1 AS Roma

AC Milan 0 Atalanta 0

Ratiba

Jumapili Desemba 18

1430 Sassuolo v Inter Milan

1700 Napoli v Torino

1700 Pescara v Bologna

1700 Udinese v Crotone

1700 Chievo v Sampdoria

2245 Genoa v Palermo

2245 Lazio v Fiorentina