REFA MIKE DEAN KUCHEZESHA SPURS-VILLA LICHA KUWA KIKAANGONI KADI NYEKUNDU YA FEGHOULI!

REFA-MIKE-DEANREFA Mike Dean antakuwa dimbani Jumapili kuchezesha Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP kati ya Tottenham Hotspur na Aston Villa licha kulalamikiwa kuhusu uamuzi wake wa kumpa Kiungo wa West Ham United kutoka Algeria Sofiane Feghouli Kadi Nyekundi kwa rafu yake dhidi ya Beki wa Manchester United Phil Jones.

West Ham imethibitisha kukataa Rufaa kupinga hiyo Kadi Nyekundu ya Feghouli na FA, Chama cha Soka England, kitatoa uamuzi wa Rufaa hiyo baadae Leo.

Feghouli, mwenye Miaka 27, amekuwa Mchezaji wa 5 kuonyeshwa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean Msimu huu.

Baada ya Mechi hiyo, Wachambuzi na Mashabiki wengi walikuja juu kuhusu uamuzi huo wa Refa Dean lakini Listi ya Marefa kwa ajili ya Mechi za FA CUP za Wikiendi hii ilikuwa tayari imeshatoka kabla ya Mechi ya Man United na West Ham.

Hadi sasa, PGMOL, Taasisi inayosimamia Marefa wa Kulipwa huko England, inaaminika haina nia kumwadhibu Dean ingawa habari za ndani zimedai wamekiri kosa la Dean.

Lakini pia inaaminika PGMOL inaelewa ni kwanini Dean alitoa Kadi Nyekundu wakiamini Dean aliona Mguu wa Feghouli uko juu na kugongana na Jones aliepiga kelele kwa maumivu matukio yote yakitokea kwa muda mfupi mno na spidi kali.

Refa Mike Dean ameshaichezesha Tottenham mara 3 Msimu huu, Mechi zote zikiwa za Ligi, na kila Mechi amempa Kadi Nyekundu Mchezaji wa Timu pinzani ya Tottenham wakiwa ni Adnan Januzaj wa Sunderland, Winston Reid wa West Ham na Nathan Redmond wa Southampton.