BLIND AFUKUZWA!

BLIND-BABA-MWANANETHERLANDS imemtimua Kocha wake Mkuu Danny Blind aliedumu kazini kwa Miaka Miwili.

Hatua hiyo inafuatia Netherlands kuchapwa 2-0 na Bulgaria Juzi Jumamosi na kuwaacha wakigalagala Nafasi ya 4 kwenye Kundi A la Nchi za Ulaya kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

Baada ya Nusu ya Mechi zote za Kundi A, Netherlamds wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 6 huku France wakuiongoza kwa kuwa na Pointi 13.WC-EURO-A

Blind, mwenye Miaka 55 na ambae Mwanawe ni Daley Blind anaechezea Manchester United na Netherlands, aliteuliwa Kocha kumrithi Guus Hidink Mwaka 2015.

Chama cha Soka cha Netherlands kimesema Matokeo yamewaacha mahala pabaya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Jumanne Netherlands itacheza Kirafiki na Italy na Timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Fred Frim.

Mara baada tamko hilo la FA ya Udachi, Daley Blind alimtumia ujumbe wa kumsapoti Baba yake Danny Blind.

DELE ALLI ‘JELA’ MECHI 3 ULAYA!

>>UEFA YAZIPIGA FAINI ARSENAL, BAYERN NA ST-ETIENNE!

DELE-ALLI-JINAKIUNGO wa Tottenham Dele Alli amefungiwa Mechi 3 za Ulaya baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu Timu yake ilipocheza na KAA Gent ya Belgium Uwanjani Wembley Mwezi Februari kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.

Alli alitolewa alipomvaa Mchezaji wa Gent Brecht Dejaegere kwenye Droo ya 2-2 na sasa UEFA imdethibitisha Adhabu yake.

Ikiwa Spurs watafuzu ndani ya 3 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, basi Alli hatacheza Mechi 3 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao na hizo ni Nusu za Mechi za Awamu hiyo.

Wakati huo huo, Arsenal nayo imepigwa Faini ya Pauni 4,300 na UEFA kwa kosa la Mashabiki wao kuvamia Uwanja wa Kuchezea walipodundwa 5-1 na Bayern Munich Uwanjani Emirates.

UEFA pia imeipiga Faini Bayern Munich ya Pauni 2,600 baada ya Mashabiki wao kusababisha Mechi hiyo na Arsenal kuchelewa kuanza waliporusha Uwanjani Mabunda ya Karatasi za Chooni wakilalamikia Bei ya Juu ya Tiketi za Viingilio.

Timu nyingine iliyopigwa Faini na UEFA ni Saint-Etienne ya France ambayo itapaswa kulipa Pauni 43,000 baada ya Mashabiki wao kufyatua Fataki za Moto Uwanjani Old Trafford Mwezi uliopita walipofungwa na Manchester United kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.

ARSENAL: SANCHEZ, OZIL KUBAKI, KUNG’OKA KUJULIKANA MWISHONI MWA MSIMU!

ARSENAL-SANCHEZ-OZILArsenal imesimamisha mazungumzo yao ya kuongeza Mikataba na Wachezaji wao Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwishoni mwa Msimu huu kwa mujibu wa Meneja Arsene Wenger.

Wachezaji hao wamabakisha Miezi 15 tu ya Mikataba yao ya sasa na Arsenal na wote wamehusishwa na kuhama.

Wakati Sanchez akiwa kimya kuhusu hatima yake, Ozil alikaririwa Mwezi Januari kuwa kubaki kwake Arsenal kunategemea kama Wenger atabakia Arsenal.

Nae Wenger Mkataba wake na Arsenal unakwisha mwishoni mwa Msimu huu na hadi sasa hamna uhakika kama atabaki au la ingawa zipo habari thabiti Arsenal ishamwekea Mezani Mkataba mpya wa Miaka Miwili.

Msimu huu, Sanchez ameifungia Arsenal Bao 22 na Ozil kupiga 9.

Juzi Wenger alitoboa ameshafikia uamuzi wake kuhusu hatima yake hapo Arsenal na kutamka atautangaza hivi karibuni.

Akiongea na beIN Sports, Wenger amesema: “Kwa sasa hatujafikia makubaliano na Wachezaji hao Wawili. Tumeamua kutilia mkazo tunamaliza vipi Msimu huu na kuzungumza kuhusu wao mwishoni mwa Msimu.”

Huko nyuma, Wenger aliwahi kusema yuko tayari kuwabakisha Arsenal Ozil na Sanchez hadi 2018 watakapomaliza Mikataba yao na kuondoka bure bila Senti kulipwa kuliko kuwauza mwishoni mwa Msimu huu.

MAN UNITED YAMRUHUSU SCHWEINI KUJIUNGA CHICAGO FIRE!

MANUNITED-SCHWEINIKIUNGO kutoka Germany Bastian Schweinsteiger ameruhusiwa na Klabu yake Manchester United kujiunga na Chicago Fire inayocheza Ligi MLS huko USA.
Schweinsteiger alijiunga na Man United iliyokuwa chini ya Louis van Gaal kutoka Bayern Munich Julai 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 14.4 lakini tangu aingie Jose Mourinho madarakani mwanzoni mwa Msimu huu Mchezaji huyo amekuwa hayupo Kikosi cha Kwanza.
Dili ya Schweini kuhamia Chicago Fire ilikamilika Jana na Uhamisho wake utakuwa rasmi baada ya kukamilisha upimwaji Afya yake na kupata Visa.
Kwa mujibu wa Gazeti Chicago Tribune la huko Marekani, Schweinsteiger, mwenye Miaka 32, amesaini Mkataba wa Mwaka Mmoja na Chicago Fire  wenye kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Schweinsteiger, ambae aliiongoza Germany kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2014, ilikuwa ahamie Chicago Fire tangu Januari lakini akaamua kubaki Man United.
Hata hivyo, Kiungo huyo amekuwa hana thamani kwa Mourinho na alicheza Mechi yake ya kwanza Msimu huu ya EFL CUP dhidi ya West Ham hapo Novemba 30.
Baada ya hapo alicheza Mechi 3 zaidi na ya mwisho ni ile dhidi ya Saint-Etienne kwenye UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 22.

WENGER AUNGAMA ARSENAL NI TAABANI, KUTANGAZA HATIMA YAKE HIVI KARIBUNI!

WENGER-HATIMAMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa atatamka kuhusu hatima yake hivi karibuni baada ya kufikia uamuzi kama atabaki Arsenal au la.EPL-MAR18A

Wenger alizungumza hayo Jana mara baada ya kutwangwa 3-1 na West Bromwich Albion huko The Hawthorns katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, hicho kikiwa ni kipigo chao cha 4 katika Mechi 5 za EPL kina kilichowatupa Nafasi ya 5 na kuhatarisha kumaliza kwao ndani ya 4 Bora kitu ambacho hakijawakuta tangu 1996.

Kipigo hicho kimeongeza presha kwa Wenger huku Mashabiki wengi wakitaka ang’oke kwenye Klabu hiyo ambayo yupo tangu 1996.

Wenger ameeleza: “Ninajua nitakachofanya. Nyie mtajua hivi karibuni!”

Wenger, mwenye Miaka 67, aliongeza: “Leo sina wasiwasi na kipigo hiki. Kwa sasa tupo katika kipindi kibaya kupita chochote kwa Miaka 20! Tunafungwa Gemu baada ya Gemu na hilo kwangu ni muhimu kuliko hatima yangu!”

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni huu na arsenal ishampa Ofa ya Mkataba Mpya wa Miaka Miwili.

Alan Shearer, Lejendari wa England, akiongea na BBC, Shirika la Utangazaji la BBC:

“Matamshi yake yanaonyesha ataondoka. Anaonekana kama Mtu alievunjika Moyo. Mitandaoni Watu wameongea mengi. Lakini Wachezaji wake hawajaongea lolote. Leo wameongea. Uchezaji wao unaonyesha hawamtaki Wenger. Uwanjani hawana Mioyo, hawapigani, hawana mwelekeo. Ukimwondoa Alexis Sanchez, wengine wote ni fedheha tupu!”