FA EMIRATES CUP: MABINGWA MAN UNITED WAPETA, ROONEY AIKAMATA REKODI, TIMU KUBWA 3 ZABWAGWA NA TIMU 'NDOGO'!!

FA-CUP-16-17-ROONEY-KOMBEMABINGWA WATETEZI wa EMIRATES FA CUP Manchester United wameanza vyema utetezi wao hapo Jana kwa kuibonda Timubya Daraja la chini Reading 4-0 huko Old Trafford katika Mechi ya Raundi ya 3 huku Nahodha wao Wayne Rooney akipachika Bao 1 na kuishika Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya Man United.
Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Man United na kufungwa Dakika ya 7 baada Rooney, akicheza Mechi yake ya kwanza baada kukosa 3 akiwa Majeruhi, kuunganisha Krosi ya Anthony Martial .
Hilo ni Bao lake la 249 kwa Man United na kumkamata Lejendari Sir Bobby Charlton aliepiga Bao 249 na kuweka Rekodi ya Mfungaji Bora Mwaka 1976.
Bao nyingine za Man United zilipachikwa na Anthony Martial na Marcus Rashford Bao 2.
Katika Mechi nyingine za hapo Jana Klabu za EPL, Ligi Kuu England, Bournemouth, Stoke City na West Bromwich Albion zilitupwa nje na Klabu za Madaraja ya chini.
Bournemouth walipigwa 3-0 na Timu ya Ligi 1 Millwall, Stoke kuchapwa kwao 2-0 na Timu ya Daraja la Championship Wolverhampton Wanderers wakati West Brom pia wakipigwa 2-1 na Timu ya Championship Derby.
++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
++++++++++++++++++++
EMIRATES FA CUP:
Ratiba/Matokeo:
**Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni isipokuwa inapotajwa
West Ham United 0-5 Manchester City
Manchester United 4-0 Reading
Accrington Stanley 2-1 Luton Town
Barrow 0-2 Rochdale
Birmingham City 1-1 Newcastle United
Blackpool 0-0 Barnsley
Bolton Wanderers 0-0 Crystal Palace
Brentford 5-1 Eastleigh
Brighton & Hove Albion 2-0 Milton Keynes Dons
Bristol City 0-0 Fleetwood Town
Everton 1-2 Leicester City
Huddersfield Town 4-0 Port Vale
Hull City 2-0 Swansea City
Ipswich Town 2-2 Lincoln City
Millwall 3-0 Bournemouth
Norwich City 2-2 Southampton
Queens Park Rangers 1-2 Blackburn Rovers
Rotherham United 2-3 Oxford United
Stoke City 0-2 Wolverhampton Wanderers
Sunderland 0-0 Burnley
Sutton United 0-0 AFC Wimbledon
Watford 2-0 Burton Albion
West Bromwich Albion 1-2 Derby County
Wigan Athletic 2-0 Nottingham Forest 
Wycombe Wanderers 2-1 Stourbridge
Preston North End 1-2 Arsenal
Jumapili Januari 8
1430 Cardiff City v Fulham
1630 Liverpool v Plymouth Argyle
Chelsea v Peterborough United             
Middlesbrough v Sheffield Wednesday             
1900 Tottenham Hotspur v Aston Villa             
Jumatatu Januari 9
2245 Cambridge United v Leeds United