RIPOTI SPESHO

ROMELU LUKAKU - KUTENGEZA HISTORIA, URITHI WAKE MWENYEWE OLD TRAFFORD!

=MOURINHO AKATAA KUMFANANISHA NA DROGBA!

Romelu Lukaku amesema anataka kutengeneza 'Historia yake mwenyewe' huko Manchester United.

MANUNITED LUKAKU MOTOLukaku, Straika kutoka Belgium mwenye Umri wa Miaka 24, alijiunga na Man United mapema Mwezi huu na tayari ashaifungia Bao 2 katika Mechi zao za kujipima wakiwa Ziarani huko USA.
Msimu uliopita, akiwa na Everton, alifunga Bao 25 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Lukaku ndie Mchezaji wa kwanza kutoka nje ya England kufunga Bao 80 kwenye EPL kabla hajatimiza Miaka 24.
Ametamka: "Mie sijakamilika..Nina kazi kubwa ya kufanya lakini upo uwezekano nikawa bora kupita sasa."
Hivi sasa, huko Man United, ameungana tena na Jose Mourinho ambae alikuwa Meneja wa Chelsea wakati Staa huyo anauzwa Julai 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 28 kwa Everton.
Wiki iliyopita Mourinho aliulizwa anawafananisha vipi Lukaku na Didier Drogba alieifungia Chelsea Bao 157 katika Mechi 341 na kutwaa EPL mara 3 na UEFA CHAMPIONZ wakati Mourinho ni Meneja huko Stamford Bridge.
Mourinho alijibu: "Sifananishi. Sifananishi hata kidogo. Mmoja ana Historia yake na mwingine ndio kwanza anaianza Historia yake!"
Nae Lukaku amesema yeye na Drogba wako tofauti kabisa.
Akiongea na BBC Sport, Lukaku ameeleza: "Drogba ni Mchezaji anaehodhi Mpira, anaelengwa katika kushambulia. Mie napenda kuwa na Mpira miguuni na kukimbia kupenya nyuma ya Difensi!"
Ameongeza: "Mimi ni Romelu Lukaku, nataka kutengeneza Historia yangu mwenyewe!"
Kuhusu kuichagua Man United badala ya Chelsea ambayo pia ilitoa Ofa sawa, Lukaku amesema kuwa maono ya Mourinho ndiyo yaliyomfanya aamue kujiunga na Man United.
Amesema: "Mazungumzo yangu na Meneja yalinipa uhakika zaidi. Alinieleza mipango yake na jinsi anavyotaka kuijenga Klabu na kutaka mie niwe sehemu ya mipango hiyo. Yeye ni Meneja ambae daima aliniamini na mie naamini kazi zake. Itakuwa ni safi sana kufanya nae kazi."
Ameongeza: "Mie nimekuwa nikifanya kazi tangu nina Miaka 11!"
Lukaku alikuwa na Miaka 16 tu na bado yuko Skuli alipoanza kucheza Mechi yake ya kwanza kama Profeshenali akiwa na Klabu ya Belgium Anderlecht.
Mwaka Mmoja baadae akawa ndio Mfungaji Bora wa Ligi na kutwaa Ubingwa.
Lukaku alijiunga na Chelsea akiwa na Miaka 18 na kuichezea Mechi 15 tu na kisha kupelekwa kwa Mkopo huko Everton.
Miaka Mitano baadae Lukaku ameweka Historia ya kuwa Mchezaji wa 5 wa Bei Ghali Duniani na aliefunga si chini ya Bao 15 za EPL kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita.
Ameeleza: "Nilifanya kazi niwe Pro tangu nina Miaka 11. Daima nimekuwa na lengo la kutwaa Makombe mengi na kuichezea Klabu kama Manchester United! Nataka niikamate fursa hii!"
LUKAKU - TAKWIMU ZAKE:
-Alipopiga Bao 2 Mwezi Machi, aliweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza wa Everton tangu Gary Lineker Mwaka 1985/86 kufunga Bao 20 katika Msimu mmoja.
-Yeye ni Mchezaji wa 4 kufunga Bao 80 za EPL kabla kufikia Miaka 24 na wengine ni Wachezaji wa Kimataifa wa England Michael Owen, Robbie Fowler na Wayne Rooney.
-Lukaku ndie alieifungia Everton Bao nyingi kwenye EPL, Bao 68, katika Historia ya Klabu hiyo.
- Yeye ni mmoja wa Wachezaji Watatu waliofunga zaidi ya Bao 10 kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita ya EPL. Wengine ni Sergio Aguero na Olivier Giroud.
 

ZANZIBAR YAPIGWA BUTI, NJE CAF

!=UANACHAMA CAF KWISHNEI, KURUDI CHINI YA MBAWA ZA TFF!
CAF 2ZANZIBAR imefutwa kama Mwanachama wa CAF kufuatia Kikao cha Shirikisho hilo la Soka Barani Afrika kilichofanyika huko Rabat, Morocco.
CAF imebaini kuwa taratibu za kuiingiza Uanachama Zanzibar CAF hazikufuatwa.
Kongresi ya CAF iliyoketi huko imepitisha maamuzi kadhaa mengine yakiwemo Taratibu za Uchaguzi, Uteuzi wa Wafanyakazi na Ukomo wa utumishi CAF uwe Umri wa Miaka 70.
Pia Kamati za CAF kupunguzwa kutoka 20 hadi 11 na kuongeza ukubwa wa Kamati Kuu toka Memba 16 hadi 23.
Kikao hicho pia kililazimika kuifuta Zanzibar Uanachama wa CAF ikiwa ni Miezi Minne tu tabgu  ikubaliwe kuwa Mwanachama kamili wa CAF na wa 55 kwenye Shirikisho hilo.
Sasa Zanzibar itapaswa kurudi tena chini ya mbawa za TFF.
Akitangaza uamuzo huo, Rais wa CAF Ahmad aliambia Kongresi hiyo: "Waliingizwa Uanachama bila kutafakari vizuri Kanuni zetu. CAF haiwezi kuwa na Wanachama Wawili toka Nchi moja. Na tafsiri ya nani ni Nchi inatoka Umoja wa Nchi Huru za Afrika, AU, na Umoja wa Mataifa, UN"
Uamuzi huu wa CAF sasa ni sawa na ule wa FIFA wa kuigomea Zanzibar kuwa Mwanachama wake kamili.

VPL – LIGI KUU VODACOM: RATIBA MSIMU MPYA 2017/18 YATOKA, KUANZA AGOSTI 26!

>FUNGUA DIMBA MSIMU: NGAO YA JAMII YANGA-SIMBA AGOSTI 23!

>KARIAKOO DABI: YANGA-SIMBA, NYERERE DEI, OKT 14!

VPL DTB SITTFF Jana ilianika Ratiba Msimu Mpya wa 2017/18 ambao utaanza rasmi kwa Mechi kufungua pazia kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa Yanga na waliobeba FA CUP Simba hapo Agosti 23.

VPL, Ligi Kuu Vodacom, itaanza rasmi Agosti 26 kwa Mechi 7 na Siku inayofuata Mabingwa Yanga kuanza utetezi wa Taji lao Jijini Dar es Salaam kwa kucheza na Timu iliyopanda Daraja Lipuli.

Ule mtanange mahsusi wa Watani wa Jadi, Yanga na Simba, sie tumeubatiza ‘Kariakoo Dabi’ ila wale wanaotukuza mambo wauita ‘Dar Dabi’, utapigwa Oktoba 14, Nyerere Dei, Siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere.

Simba watafungua Msimu wao wa VPL kwa kucheza Nyumbani na Ruvu Shooting hapo Jumamosi ya Agosti 26.

Michezo mingine ya Siku ya Ufunguzi, Jumamosi ya Agosti 26, itawakutanisha Ndanda wakiwa Wenyeji wa Azam FC wakati Mwadui ikiwakaribisha wapya Singida United, huku Mtibwa ikicheza Nyumbani na  Stand United.

Huko Bukoba, Kagera Sugar watakuwa Wenyeji wa Mbao FC na Timu Mpya Njombe Mji ikiwa Nyumbani kuivaa Tanzania Prisons.

Mechi nyingine ya Siku ya Ufunguzi ni huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya wakati wa Nyumbani Mbeya City wakikipiga na Majimaji FC.

VPL, LIGI KUU VODACOM

Mechi za Ufunguzi

Jumamosi 26/08/2017

Ndanda v Azam

Mwadui v Singida

Mtibwa v Stand

Simba v Ruvu

Kagera v Mbao

Njombe v Prisons

Mbeya v Majimaji

Jumapili, 27/08/2017

Yanga v Lipuli

**RATIBA KAMILI YA MSIMU WOTE TUTAIRUSHA BAADAE

EXCOMM YA TFF YABADILI KAMATI ZAKE, SASA ZASHEHENI MAWAKILI!

>PATA TAARIFA KAMILI:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JULAI 04, 2017

UAMUZI WA KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI

TFF TOKA SITKamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana tena leo Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kamati hiyo ya utendaji inakutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.

Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.

Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.

Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.

Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.

Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi - ASP Benedict Nyagabona.

Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.

………………………………………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TFF UCHAGUZI-29 WAFANYIWA USAILI SIKU YA KWANZA, 19 WAHITIMU UKOCHA BEJI A CAF!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                   JUNI 29, 2017

MAKOCHA 19 WAHITIMU KOZI DARAJA ‘A’ YA CAF

Makocha 19 wa mpira wa miguu, wamehitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

TFF TOKA SITMakocha hao walimaliza gwe ya pili ya siku 19, katika kozi hiyo ambayo mbali ya kuwa na wakufunzi wengine, wakufunzi wakuu wa CAF walikuwa ni Athumani Lubowa na Sunday Kayuni.

Kayuni ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa TFF katika kozi hii amehudumu kama mkufunzi mkuu wa CAF na aliyekuja kuwasimamia (Accessor) ni Mkurugenzi wa sasa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda, Athumani Lubowa.

Makocha waliohitimu ni Kidao Wilfred Mzigama, Ali Vuai Shein, Wane Nelson Mkisi, Abdulmutik Haji Ali, Hababuu Ali Omar, Meck Maxime Kianga, Salim Ali Haji, Malale Hamsini Keya na Abdallah Mohammed Juma.

Wengine ni Salim Juma Makame, Emmanuel Raymond Massawe, Mohammed Alawdin Tajdin, Fikiri Elias Mahiza, Juma Ramadhani Mgunda na Dismas Gordon Haonga, Abdul Hassan Banyai, Maka Andrew Mwalwisi, Dennis Mrisho Kitambi na Sebastian Leonard Nkoma.

Akifunga kozi hiyo, Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Khalid Mohammed Abdallah aliwatakia kila la kheri kwa makocha hao akiwaelezea kuwa wamejaa utajiri wa ufundi ambao hawana budi kuutendea haki kwa kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu.

Awali, akizungumzia wahitimu hao, Mkufunzi Lubowa alisema kwamba anamini makocha hao watafanya vema kwa kuwa katika kipindi chote cha kozi, walionyesha kuwa na nidhamu ya hali ya juu - alama kuu ya mafanikio.

USAILI WAGOMBEA TFF

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya usaili kwa wagombea 29 wa nafasi mbalimbali katika siku ya kwanza ya hatua hiyo muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho.

Kabla ya usaili, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli, aliwatangazia wagombea wote kuwa amepokea mapingamzi mawili ambayo ni:-

Hussein Mwamba ambaye ni Mjumbe kwa sasa wa Kamati ya Utendaji ya TFF, aliyempinga Mussa Sima kuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo katika Kanda ya 10 ya Mikoa ya Dodoma na Singida kuwa hana uzoefu wa miaka mitano.

Wanafamilia wote kwa maana ya Mwamba na Sima walikuwako. Wakaitwa kikaoni, lakini mweka pingamizi - Mwamba aliamua kulitoa pingamizi lake.

Pingamizi jingine ambalo liliwekwa leo ni kwa Mgombea nafasi ya urais John Kijumbe ambaye anapinga Wallace Karia - Makamu Rais kwa sasa wa TFF kwamba hana sifa za kuwania urais wa TFF kama alivyoomba.

Hata hivyo, pingamizi hilo halijasikilizwa kwa sababu ya wahusika wote kutokuwako na baada ya kamati kufanya nao mawasiliano, wametangaza kusikiliza pingamizi hilo Jumamosi ambayo ni siku ya mwisho ya usaili.

Wagombea ambao wamesailiwa leo hadi jioni ya leo Alhamisi kwa upande wa wagombea urais ni Imani Madega na Ally Mayay wakati Wagombea Makamu urais waliosailiwa ni Mtemi Ramadhani na Mulamu Nghambi.

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum Chama

Kaliro Samson

Leopold Mukebezi

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Aaron Nyanda

Samwel Daniel

Bado

Vedastus Lufano

Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Mbasha Matutu

Bado

Benista Rugora

Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Wote Bado

Omari Walii

Sarah Chao

Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John Kadutu

Bado

Issa Bukuku

Abubakar Zebo

Francis Michael

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Baraka Mazengo

Bado

Kenneth Pesambili

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

Elias Mwanjala

Cyprian Kuyava

Bado

Erick Ambakisye

Abousuphyan Silliah

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

Wote bado

James Mhagama

Golden Sanga

Vicent Majili

Yono Kevela

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Wote Bado

Athuman Kambi

Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

Hussein Mwamba

Mohamed Aden

Musa Sima

George Benedict Komba

Bado

Stewart Masima

Ally Suru

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Gabriel Mkwawe

Bado

Charles Mwakambaya

Francis Ndulane

Hassan Othman ‘Hassanol’

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Khalid Mohamed

Bado

Goodluck Moshi

Thabit Kandoro

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

Emmanuel Ashery

Shaffih Dauda

Mussa Kisoky

Lameck Nyambaya

Jamhuri Kihwelo

Saad Kawemba

Bado

Bakari Malima

Ayoub Nyenzi

Saleh Alawi

Ramadhani Nassib

Aziz Khalfan

Abdul Sauko

Peter Mhinzi

Ally Kamtande

Said Tully

……………………………………………………………………………………………..

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA