HULL YAMTIMUA PHELAN, BAADA ARSENAL KUNUSURIKA, ‘KIKOSI CHA WENGER NJE’ CHAREJEA KAZINI!

HULL-PHELANHUKU Hull City ikithibitisha kuachana na Meneja wao Mike Phelan, huko Arsenal Mashabiki wameanza tena kunyanyua Bango la kumtaka Meneja wao Arsene Wenger ang’oke.

HULL CITY – YAMTIMUA MIKE PHELAN!

KLABU ya Hull City imethibitisha kuachana na Meneja wao Mike Phelan alieshinda Mechi 3 tu kati ya 20.WENGER-WIMA

Phelan, mwenye Miaka 54 na ambae alikuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Man United, aliteuliwa Meneja wa kudumu Mwezi Oktoba.

Juzi Jumatatu, Hull City ilichapwa 3-1 na West Bromwich Albion na kuiacha ikiwa eneo la hatari la mkiani mwa EPL, Ligi Kuu Engl, wakiwa na Pointi 13 kwa Mechi 20.

Phelan aliteuliwa Meneja wa Muda wa Hull mwanzoni mwa Msimu kuchukua Nafasi ya Steve Bruce ambae aliamua kuachana na Klabu hiyo ikiwa ni Miezi Miwili tu tangu aipandishe Daraja.

Msimu huu, Hull walianza vyema EPL kwa kushinda Mechi zao 2 za kwanza dhidi ya Mabingwa Watetezi Leicester na Swansea lakini baada yah apo wakadorora.

BAADA ARSENAL KUNUSURIKA, ‘KIKOSI CHA WENGER NJE’ CHAREJEA KAZINI!

Jana Arsenal ililazimisha Sare ya 3-3 na Bournemouth huko Vitality Stadium katika Mechi ya EPL baada ya kutanguliwa 3-0 lakini Matoke ohayo yameamsha hasira za Mashabiki wa Arsenal Duniani kote na kumtaka Meneja wao Arsene Wenger atimke.

Vilio vya Mashabiki hao vilichomoza toka kila pembe ya Dunia kote kwenye Mitandao ya Kijamii.

Ingawa Arsenal walijitutumua mwishoni mwa Mechi hiyo ambayo walicheza ovyo mwanzoni na kuzinduka Dakika 20 za mwisho na kurudisha Bao zote 3 lakini hasira za Mashabiki zilikuwa kubwa mno.

PATA BAADHI YA MANENO YA MASHABIKI HAO KWENYE TWITTER:

ARSENAL-WENGER-OUT-BRIGADE