MOURINHO: ‘BADO HATUJAPATA OFA ZA KURIDHISHA KWA MORGAN SCHNEIDERLIN NA MEMPHIS DEPAY’

MANUNITED-SCHNEIDERLIN-DEPAYWACHEZAJI WAWILI wa Manchester United, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay, hawatakuwemo kwenye Vikosi vya Mechi za Timu yao hadi ijulikane nini hatima yao kwa mujibu wa Meneja Jose Mourinho.

Wawili hao hawajaichezea Man United tangu Novemba huku wakihusishwa na kuihama Timu hiyo kwenye Dirisha la Uhamisho la hii Januari.

Inategemewa Schneiderlin, mwenye Miaka 27, atakwenda Everton.

Lakini Mourinho amesema: “Ntawaruhusu wote Wawili kuondoka ikiwa tutapa Ofa safi. Hadi sasa hamna Ofa hiyo! Hatujapata Ofa inayolingana na ubora wa uchezaji wao!”

Jumamosi Man United wanacheza na Reading kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP Uwanjani Old Trafford na Mourinho amesema hali ingekuwa kawaida Wachezaji hao Wawili wangekuwemo kwenye Kikosi cha Mechi hiyo.

Mourinho ameeleza: “Hawamo Kikosini kwa sababu tulikuwa tukingoja kitu ambacho Wiki kadhaa nyuma kilionekana kipo tayari Asilimia 100 lakini sasa ni Asilimia 0!”

Mbali ya Everton kumtaka Schneiderlin, West Bromwich Albion pia ilitoa Ofa ya Pauni Milioni 15 kumnunua na kukataliwa.

Vile vile Everton inamtaka Winga Depay, mwenye Miaka 22, ingawa pia Klabu kadhaa za Ulaya pia zinatajwa.