BARCA YAKWAMA KUMUONGEZA DAU MESSI!

==KWA SASA, NEYMAR, SUAREZ WAZOA MKWANJA JUU KUPITA MESSI!
BARCA-MESSI-TODOSOMOSMKURUGENZI MTENDAJI MKUU wa FC Barcelona, Òscar Grau, ametoboa kuwa kwa sasa wameshindwa kumpa Lionel Messi Mkataba mpya baada kubanwa na Kanuni za La Liga.
Kwa sasa, Mkataba wa Messi unaokwisha baada ya Miezi 18, unampa Mshahara wa Euro Milioni 22 kwa Mwaka baada kukatwa Kodi.
Lakini wenzake, Neymar na Luis Suarez, ambao hivi karibuni walisaini Dili Mpya zinazoisha 2021, wanazoa kitita cha Euro Milioni 25 kwa Mwaka baada ya Kodi.
Mkataba wa Messi unamalizika Tarehe 30 Juni 2018 na baada ya hapo yupo huru kuondoka bila Barca kulipwa hata Senti.
Barca wamekwama kumuongeza Messi Mshahara kwa vile wanabanwa na Kanuni za La Liga zinazotaka kila Klabu kutozidi Asilimia 70 ya Bajeti yao kwa kulipia Mishahara.
Oscar Grau ameeleza: "Barcelona inabidi iwe makini. Barca hairuhusiwi kuvuka Asilimia 70 ya Bajeti kwa kulipia Mishahara!"
Kwa mujibu wa Takwimu, Barca ndio wanaolipa Mishahara mikubwa huko Spain na Duniani ni wa Pili nyuma ya Manchester United.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Barca, Grau, amedokeza kuwa watapaswa kuuza Wachezaji na pia kuimarisha Mapato ya Kibiashara ikiwa watataka kuvuna Fedha zaidi ili kuboresha Maslahi ya Wachezaji waliopo.