MOURINHO ANENA MAN UNITED SASA IKO NGANGARI MBIO ZA UBINGWA ENGLAND!

==ILA ULAYA....MAMBO BADO!!
MANUNITED MOU PLAYERS TRAININGManchester United sasa wana 'zana bora' za kutwaa Ubingwa wa England Msimu huu mpya unaoanza Agosti lakini kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI bado wanahitajika kuwa 'bora zaidi' kwa mujibu wa Meneja wao machachari Jose Mourinho.
Msimu uliopita, ukiwa ni Msimu wa kwanza kwa Mourinho kushika hatamu Old Trafford, Man United walitwaa Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi, EFL CUP,  na UEFA EUROPA LIGI ambalo limewawezesha kuingizwa Makundi ya UCL Msimu huu ujao licha kushika Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Akihojiwa na BBC Sport hapo Jana kama Man United wanalenga kutwaa Ubingwa wa EPL Msimu huu mpya, Mourinho alijibu: "Sasa tupo tayari zaidi!"
Kwa ajili ya Msimu mpya, Man United imewasajili Wachezaji Wapya Romelu Lukaku na Victor Lindelof.
Mourinho ameeleza: "Msimu utakuwa mgumu lakini nadhani sasa tupo imara zaidi kupigania Ubingwa. Nadhani sasa tuna zana bora zaid. Lakini tunapigana na Timu bora zaidi zilizowekeza bora zaidi. Lakini nakiamini Kikosi changu, ari yetu, nia yetu, mshikamano wetu. Nawaamini Vijana wangu na tutajaribu!"
Aliongeza: "Tulienda EUROPA LIGI.kama moja ya Timu kubwa, sasa tunaenda CHAMPIONZ LIGI na hatupo kwenye Timu kubwa. Inabidi tufanye vyema zaidi huko. Kitu muhimu ni kusaka Timu yenye furaha na kuelewana."
Pia alisema: "Nina furaha na Kikosi changu lakini napenda kuongeza Wachezaji Wawili zaidi. Kiungo atanipa uwezo zaidi wa kutumia mifumo na mbinu nyingi zaidi. Mwingine ni Fowadi anaeshambulia toka kwenye Wingi ili nipate upana zaidi wa mashambulizi."
Mourinho amesisitiza hana wasiwasi na kupata hao wapya na yeye anasubiri 'habari njema' tu toka kwa Mtendaji Mkuu Ed Woodward.

CONTE ATOBOA PEDRO 'KAVUNJIKA MIFUPA' KADHAA BAADA DHORUBA YA KIPA DAVID OSPINA!

PEDRO OSPINA DHORUBAKwa mujibu wa Meneja wa Chelsea Antonio Conte Fowadi wao Pedro aliegongana na Kipa wa Arsenal David Ospina walipokuwa wakigombea Mpira kwenye Mechi kati yao huko Beijing, China hapo Juzi amekutwa na nyufa kadhaa kwenye Fuvu lake.
Conte amesema Pedro kwa sasa anapaswa kuvaa kinga maalum Kichwani kwa Siku 10 ili kuilinda sehemu iliyoumia.
Conte ameeleza:"Hali ni tete lakini akivaa kinga maalum Usoni na Kichwani kwa muda wa Siku 10 anaweza kurejea Kikosini."
Pedro, Raia wa Spain, alivamiwa na Kipa Ospina ndani ya Penati Boksi Jumamosi iliyopita wakati Chelsea inaitandika Arsenal 3-0.
Pedro alitolewa Uwanjani Bird's Nest akiwa na kizunguzungu na kupepesuka huku akiwa na michubuko kadhaa Usoni na Kichwani.
Ilibidi Siku ya Pili Pedro arudishwe Makao Makuu ya Chelsea Jijini London Nchini England kutokea huko Beijing ili kutibiwa dhoruba hiyo ya Kichwani iliyomletea maluweluwe.
Msimu uliopita, Pedro aliifungia Chelsea Bao 13 katika Mechi 43 na pia kuiwezesha Timu hiyo kutwaa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND.

CONTE AMTEUA GARY CAHILL KEPTENI CHELSEA!

CHELSEA CAHILLMENEJA wa Chelsea Mabingwa wa England, Antonio Conte, amethibitisha kuwa Gary Cahill ndie Kepteni wao mpya kuchukua nafasi iliyoachwa na mstaafu John Terry.
Terry alishika Unahodha tangu 2004 hadi alipoondoka Chelsea mwishoni mwa Mwezi uliokwisha baada kumaliza Mkataba wake.
Msimu uliopita, mara nyingi Cahill alivishwa Utepe wa Unahodha kwa vile Terry alikuwa hana namba ya kudumu Kikosini.
Wengi walitarajia Cahill ndie atakuwa mrithi wa Terry lakini David Luiz na Cesar Azpilicueta pia walitajwa kuwa na uwezo wa kuchukua wadhifa huo.
Licha kusisitiza Cahill ndie Kepteni, Conte amewataka Wachezaji wake wote wengine Kikosini kudhihirisha wao pia ni Makepteni.
Ameeleza: "Nadhani tunao Makepteni wengine na wanaweza kuwa Azpilicueta, Luiz, na baadae inaweza kuwa Thibaut Courtois, Cesc Fabregas!"

LIVERPOOL YAIBWAGA LECESTER NA KUTWAA ASIA TROPHY HUKO HONG KONG!

LIVER LEILiverpool Leo huko Hong Kong wametoka nyuma kwa Bao 1 na kuichapa Leicester City 2-1 na kubeba Premier League Asia Trophy.
Leicester ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 12 baada ya Krosi ya Christian Fuchs kuunganishwa kwa Kichwa na Islam Slimani na kumpita Kipa Loris Karius.
Mohamed Salah akaisawazishia Liverpool Dakika 8 baadae na ilipobaki Dakika 1 kwenda Haftaimu Philippe Coutinho aliachia kigongo kilichomshinda Kipa Kasper Schmeichel na kuwapa Liverpool ushindi wa 2-1.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Liverpool: Karius; Alexander-Arnold, Matip, Lovren, Milner; Wijnaldum, Lallana, Coutinho; Salah, Firmino, Origi
Leicester: Schmeichel, Morgan, Drinkwater, Vardy, Albrighton, Maguire, Amartey, Slimani, James, Mahrez, Fuchs
 

JOSE MOURINHO ATAKA ANGALAU MPYA MMOJA ASAINIWE HARAKA!

MANUNITED MOURINHO LINDELOFJose Mourinho ameitaka Manchester United kusaini angalau Mchezaji Mmoja Mpya haraka iwezekanavyo.

Alfajiri ya Leo, huko Houston, Texas, USA, Mourinho alishuhudia Wachezaji wake Wapya Wawili, Romelu Lukaku and na Victor Lindelof, wakicheza walipowafunga Mahasimu wao Man City 2-0 katika Mechi ya International Champions Cup na kusema amefurahishwa na uchezaji wa Wapya hao huku Lukaku akifunga Bao 1.

Mourinho ameeleza: “Tukipata Mchezaji mmoja zaidi, haraka iwezekanavyo itakuwa vyema, Angalia Lindelof yuko kwenye Timu, Lukaku yuko kwenye Timu, wanacheza vizuri!”

Mourinho ameeleza kuwa jinsi Timu nyingine za EPL, LIGI KUU ENGLAND, zilivyosajili ni muhimu kwao kuimarisha Kikosi chao zaidi.

Alipoulizwa ikiwa Man United itasaini Mchezaji Mpya wa 3 kabla kuondoka USA, Mourinho alijibu: “Sijui, sijui. Si mimi ninaedhibiti hilo. Sifa kwa Lukaku, Lindelof kuwa humu haraka si yangu, ni ya Ed Woodward [Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United] na timu yake. Namshukuru kwa kazi njema kutuletea Wachezaji hawa Wawili muhimu lakini tunahitaji wengine.”

Aliongeza: “Ukiangalia Timu nyingine za Ligi Kuu jinsi wanavyopata wapya, Wachezaji wazuri na ona Mabingwa Chelsea wamenunua Wachezaji Wazoefu Watatu, City wapo sokoni, Liverpool na West Ham wamewapata Joe Hart, Chicharito na Arnautovic. West Ham nao wanashindana EPL. Timu zipo sokoni mie bado nangoja!”

Man United bado wamebakiza Mechi 2 za Ziara yao huko USA ambapo watacheza na Real Madrid Jumapili huko Santa Clara na kisha Wiki ijayo kucheza na Barcelona.

Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]

17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah [2-1]

20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup) [2-0]

23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)

26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)

30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo

2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin

8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)