MWAKA MPYA: JUMAPILI ARSENAL v PALACE, WENGER AMHOFIA BIG SAM!

WENGER-BIGSAMArsene Wenger amekiri kuwa Mpinzani wake wa Siku nyingi Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, ni hatari kubwa katika azma ya Arsenal kufufua matumaini yao kwenye mbio za Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England.

Sam Allardyce hivi sasa ndio Meneja Mpya wa Crystal Palace ambayo Jumapili Januari Mosi, 2017, Siku ya Kwanza ya Mwaka Mpya, itazuru Emirates kucheza na Arsenal Mechi ya EPL.

Huko nyuma, wakati Allardyce akiwa Meneja wa Bolton Wanderers na West Ham, Wenger ashawahi kukwaruzana nae.

Hivi sasa Arsenal wako Nafasi ya 4 kwenye EPL na Mechi hii na Palace ni muhimu mno kwa Wenger na Arsenal yake kushinda ili wasitupwe mbali kwenye mbio za Ubingwa.

Lakini, kama ambavyo Wenger anavyotambua, Siku zote Timu za Big Sam hutumia miguvu na Mipira ya moja kwa moja bila kulemba ili kuwayumbisha Arsenal wanaopenda kumiliki mno Mpira.EPL-DEC31A

Kwa Allardyce hii itakuwa Mechi yake ya Pili kuiongoza Palace tangu ateuliwe kuwa Meneja Wiki moja iliyopita nay a kwanza ilikuwa Droo ya 1-1 na Watford Siku ya Boksing Dei.

Nao Arsenal walishinda Mechi yao ya Boksing Dei 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion kwa Bao la mwishoni lakini kabla yah apo walichapwa Mechi 2 mfululizo na Everton na Manchester City.

Wenger, akiongea kuelekea Mechi hii na Palace, ameonyesha waziwazi kuihofia Mechi hii kwa kusema: “Ni muhimu mno kwa kila Timu kupigana kuwa juu. Baada ya kupata Meneja Mpya ni wazi Palace watajiamini zaidi na kuwa na mori zaidi. Hilo litafanya Gemu iwe ngumu mno. Chini ya Allardyce, Palace ni hatari mno!”

Arsenal wako Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea na ushindi dhidi ya Palace ni kitu cha kufa na kupona kwao.

Hali za Wachezaji

Arsenal huenda wakamkosa Theo Walcott ambae ana maumivu ya Musuli za Mguu akiungana na Majeruhi Kieran Gibbs mwenye tatizo la Goti lakini Sentahafu Shkodran Mustafi ameshapona tatizo la Musuli za Pajani.

Pia Wenger ameshatoboa kuwa Fowadi wao Danny Welbeck amepona tatizo la Goti lililomweka nje kwa muda mrefu na amerejea Mazoezini lakini kilichobaki ni kuamua ni wakati gani muafaka kuanza kumtumia tena.

Kwa upande wa Palace, wao watamkosa Beki wao Damien Delaney ambae yuko Kifungoni.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

ARSENAL: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Coquelin, Xhaka, Sanchez, Ozil, Iwobi, Giroud

Akiba: Ospina, Martínez, Jenkinson, Gabriel, Holding, Elneny, Ramsey, Reine-Adélaïde, Sanogo, Pérez

CRYSTAL PALACE: Hennessey, MacArthur, Dann, Kelly, Ward, Flamini, Puncheon, Zaha, Cabaye, Townsend, Benteke

Akiba: Speroni, Fryers, Phillips, Wynter, Sako, Lee, Husin, McArthur, Ledley, Mutch, Campbell, Tomkins, Rémy

REFA: Andre Marriner

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea