EPL: ARSENAL YAANZA MWAKA MPYA VYEMA, YASHIKA NAFASI YA 3!

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumapili Januari 1

Watford 1 Tottenham Hotspur 4            

Arsenal 2 Crystal Palace 0           

+++++++++++++++++++++++++++++

ARSE-PALACELEO Arsenal wameanza vyema Mwaka Mpya 2017 kwa kuichapa Crystal Palace 2-0 huko Emirates na kukamata Nafasi ya Tatu kwenye EPL, Ligi Kuu England.

EPL, ambayo sasa imeshachezwa Mechi 19 kati ya 38 za Msimu mzima, inaongozwa na Chelsea wenye Pointi 49 wakifuata Liverpool wenye 43, kisha Arsenal wenye 40 na kufuatia Tottenham na Man City zenye 39 kila mmoja huku ya 6 ikiwa Man United yenye Pointi 36.

Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud kwa Kisigino katika Dakika ya 17 na kudumu hadi Mapumziko.EPL-JAN1

Arsenal wakapiga Bao la Pili Dakika ya 56 kupitia Alex Iwobi.

Katika Mechi ya kwanza ya EPL iliyochezwa hii Leo, Harry Kane na Dele Alli alipiga Bao 2 kila Mtu wakati Tottenham ikiwatwanga Watford waliodorora 4-1 na kutinga kwenye 4 Bora ya EPL kwamara ya kwanza tangu Oktoba.

EPL itaendelea tena Kesho Jumatatu kwa Mechi 6.

VIKOSI:

Arsenal: Cech; Bellerín, Gabriel, Koscielny, Monreal; Elneny, Xhaka; Lucas Pérez, Iwobi, Sánchez; Giroud.

Akiba: Ospina, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Mustafi, Reine-Adélaïde, Coquelin, Maitland-Niles.

Crystal Palace: Hennessey; Ward, Dann, Tomkins, Kelly; Flamini, Puncheon, Cabaye; Townsend, Zaha, C Benteke.

Akiba: Speroni, Campbell, Lee, Fryers, Mutch, Sako, Husin.

REFA: Andre Marriner

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea