EMIRATES FA CUP – RAUNDI YA 3: LIVERPOOL YAKWAMA KWA TIMU YA DARAJA LA 4, CHELSEA, SPURS ZASONGA!

>DROO MECHI ZA RAUNDI YA 4 JUMATATU!

EMIRATES-FACUP-2017Raundi ya 3 ya FA CUP imeendelea Leo kwa Mechi kadhaa na Chelsea, Tottenham na Middlesbrough kutinga Raundi ya 4 lakini Liverpool wakiwa kwao Anfield walitoka Sare 0-0 na Timu ya Ligi 2, Plymouth Argyle na sasa wakabiliwa na Marudiano Ugenini huko Home Park, Plymouth.

Ligi 2 ni Daraja ni la 4 likiwa chini ya EPL, Ligi Kuu England, ikifuata Championship na Ligi 1.

Lakini, Liverpool, wakitumia Chipukizi wengi, walishindwa kuipenya ngome ngumu ya Plymouth licha kutawala Mechi yote. 

Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, waliitandika Timu ya Daraja la chini Peterborough United 4-1 na kubaki Mtu 10 wakiwa mbele 4-0 baada Nahodha wao John Terry kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 67.

Chelsea walifunga Bao zao kupitia Pedro Dakika za 18 na 75, Batshuayi, 43', na Willian, 52, huku Peterborough wakipata Bao lao Dakika ya 70 Mfungaji akiwa Nichols.

Middlesbrough wamewanyuka Sheffield Wednesday 3-0 licha kucheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 59 kufuatia Kadi Nyekundu ya Ayala na ushindi huo ulitokana na Bao za Dakika za 58, 67 na 91 zilizofungwa na Leadbitter, Negredo na De Roon.

++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

+++++++++++++++++++

Wakiwa kwao White Hart Lane, Tottenham wameichapa Aston Villa 2-0 kwa Magoli yaliyofungwa na Ben Davies na Song Heung-min katika Dakika za 71 na 80.

Kesho ipo Mechi 1 tu nay a mwisho ya Raundi ya 3 kati ya Cambridge United na Leeds United na mara baada ya Mechi hiyo kwisha Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 itafanyika.

EMIRATES FA CUP:

Ratiba/Matokeo:

**Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni isipokuwa inapotajwa

Ijumaa Januari 6

West Ham United 0 Manchester City 5             

EMIRATES FA CUP:

West Ham United 0-5 Manchester City

Manchester United 4-0 Reading

Accrington Stanley 2-1 Luton Town

Barrow 0-2 Rochdale

Birmingham City 1-1 Newcastle United

Blackpool 0-0 Barnsley

Bolton Wanderers 0-0 Crystal Palace

Brentford 5-1 Eastleigh

Brighton & Hove Albion 2-0 Milton Keynes Dons

Bristol City 0-0 Fleetwood Town

Everton 1-2 Leicester City

Huddersfield Town 4-0 Port Vale

Hull City 2-0 Swansea City

Ipswich Town 2-2 Lincoln City

Millwall 3-0 Bournemouth

Norwich City 2-2 Southampton

Queens Park Rangers 1-2 Blackburn Rovers

Rotherham United 2-3 Oxford United

Stoke City 0-2 Wolverhampton Wanderers

Sunderland 0-0 Burnley

Sutton United 0-0 AFC Wimbledon

Watford 2-0 Burton Albion

West Bromwich Albion 1-2 Derby County

Wigan Athletic 2-0 Nottingham Forest

Wycombe Wanderers 2-1 Stourbridge

Preston North End 1-2 Arsenal    

Jumapili Januari 8

Cardiff City 1 Fulham 2     

Liverpool 0 Plymouth Argyle 0     

Chelsea 4 Peterborough United 1          

Middlesbrough 3 Sheffield Wednesday 0          

Tottenham Hotspur 2 Aston Villa 0                  

Jumatatu Januari 9

2245 Cambridge United v Leeds United 

TAREHE MUHIMU:

HATUA

RAUNDI

DROO

MECHI

Raundi za Awali

Raundi ya Awali kabisa

8 Julai 2016

6 Agosti 2016

Raundi ya Awali

20 Agosti 2016

Raundi ya 1 Mchujo

15 Agosti 2016

3 Septemba 2016

Raundi ya 2 Mchujo

5 Septemba 2016

17 Septemba 2016

Raundi ya 3 Mchujo

19 Septemba 2016

1 Oktoba 2016

Raundi ya 4 Mchujo

3 Oktoba 2016

15 Oktoba 2016

Mashindano rasmi

Raundi ya 1

17 Oktoba 2016

5 Novemba 2016

Raundi ya 2

7 Novemba 2016

3 Desemba 2016

Raundi ya 3

5 Desemba 2016

7 Januari 2017

Raundi ya 4

Kujulishwa

28 Januari 2017

Raundi ya 5

Kujulishwa

18 Februari 2017

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

Kujulishwa

11 Machi 2017

Nusu Fainali

Kujulishwa

22 na 23 Aprili 2017

FAINALI

27 Mei 2017