UJIO WA JESUS CITY WAZONGWA NA UKIRITIMBA!

JESUSULE Uhamisho wa Mbrazil Gabriel Jesus kwenda Manchester City bado haujapata Saini ya mwisho ingawa Meneja Pep Guardiola anatarajia utakamilika kabla hawajasafiri kwenda Liverpool Jumapili kucheza na Everton huko Goodison Park kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

City walishafikia makubaliano na Klabu ya Brazil Palmeiras tangu Mwezi Julai Mwaka Jana kumnunua Kinda huyo wa Brazil mwenye Miaka 19 kwa Dau la Pauni Milioni 27 na pia kukubali Mchezaji huyo abakie Palmeiras hadi Msimu wa Brazil utakapoisha Mwezi Desemba.

Jesus amekuwa Kambini na City kwa Wiki 2 sasa lakini ukiritimba umekwamisha Uhamisho wake kukamilika rasmi na hivyo kusitisha kuichezea rasmi City.

Kinda huyo ndio kwanza amechomoza kwenye Soka la Dunia akiwa na Msimu wa Pili tu na Palmeiras lakini akaiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Taifa Mwezi Novemba baada ya kutwaa Medali ya Dhahabu akiichezea Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki, RIO 2016, Mwezi Julai.

Jesus alianza kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Taifa ya Brazil Mwezi Septemba Mwaka Jana na kufunga Bao 4 katika Mechi zake 6.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumamosi Januari 14

1530 Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion     

1800 Burnley v Southampton               

1800 Hull City v Bournemouth              

1800 Sunderland v Stoke City               

1800 Swansea City v Arsenal                

1800 Watford v Middlesbrough             

1800 West Ham United v Crystal Palace           

2030 Leicester City v Chelsea                

Jumapili Januari 15

1630 Everton v Manchester City

1900 Manchester United v Liverpool