RED BULL ARENA, USA: AS ROMA YAIZIDI SPURS!

ROMA SPURSAS ROMA ya Italy imeichapa Tottenham Hotspur ya England 3-2 katika Mechi iliyochezwa huko Red Bull Arena, USA ya Mashindano ya International Champions Cup.

Roma walianza kufunga Dakika ya 13 kwa Penati ya Diego Perotti iliyotolewa na Refa wa USA Hilario Grajeda baada ya Cameron Carter-Vickers kuunawa Mpira na Cengiz Under kupiga Bao la Pili Dakika ya 70.

Spurs wakasawazisha Bao hizo 2 kwa Bao za ndani ya Dakika 4 zilizofungwa na Harry Winks, Dakika ya 87 na Vincent Janssen Dakika ya 91.

Bao la 3 na la ushindi kwa AS Roma lilifungwa Dakika ya 92 na Marco Tumminello.

Mechi inayofuata kwa Spurs sasa ni kuwavaa wenzao wa England Manchester City huko Tennessee hapo Julai 29 kabla kuwa Wenyeji wa Juventus huko Wembley Stadium Jijini London.

Msimu Mpya Spurs watatumia Wembley kama Uwanja wa Nyumbani kwa vile Uwanja wao White Hart Lane upo kwenye Matengenezo makubwa.

NABY KEITA AUMIZA MWENZIE ZOEZINI LEIPZIG KUFOSI KUHAMIA LIVERPOOL!

==MAZOEZI YAVUNJWA!
NABY KEITAMLENGWA wa Liverpool Naby Keita amesababisha Mazoezi ya Timu yake RB Leipzig ya Germany kuvunjika baada ya kudaiwa kumchezea 'Rafu mbaya mno' mwenzake.
Ripoti toka Germany zimedai Wachezaji wote waliokuwa Mazoezini huko Nchini Austria waliamriwa wavunje Mazoezi hayo na Kocha wao Ralph Hasenhuttl kufuatia Rafu mbaya ya Keita kwa mwenzake Diego Demme na kurejeshwa Hotelini kwao.
Imedaiwa Demme alilia kwa maumivu baada ya dhoruba ya Keita na baada kupewa Huduma ya Kwanza aliondolewa Uwanja wa Mazoezi akiwa na Bendeji kubwa kwenye Goti lake la Kulia.
Kitendo hicho kinachodaiwa cha kusudi kinahisiwa ni hasira za Mchezaji huyo kutoka Guonea anaetaka kuhamia Liverpool ya England wakati RB Leipzig imekataa kabisa kumuuza.
Klabu hiyo inayocheza Bundesliga ishathibitisha kuikataa Ofa ya Pauni Milioni 66 ya kumnunua Keita iliyotolewa na Liverpool ikiwa ni Ofa yao ya 3 kukataliwa.

BIRD”S NEST STADIUM, BEIJING, CHINA: MABINGWA CHELSEA WAIBONDA ARSENAL!

ARSE CHE2LEO Mabingwa wa England Chelsea wameshuka Bird’s Nest Stadium Mjini Beijing Nchini kucheza Mechi yao ya kwanza kabisa ya kujiweka sawa na Msimu Mpya kwa kupambana na Arsenal waliokuwa tayari wana Mechi 3 kibindoni na Matokeo ni Chelsea 3 Arsenal 0.
Arsenal, wakiwa wamecheza Mechi 2 huko Australia na 1 Shanghai, China dhidi ya Bayern Munich waliyotoka Sare 1-1 na kushinda kwa Penati 3-2, wanatinga kwenye Mechi hii ikiwa ni Wiki 8 tu tangu wawabwage Chelsea kwenye Fainali ya FA CUP Uwanjani Wembley Jijini London, walijikuta wako nyuma kwa Bao 1-0 katika Dakika ya 40 alilofunga Willian baada ya kupokea Pasi ya Michy Batshuayi.
Chelsea wakaenda 2-0 mbele katika Dakika ya 42 baada ya Kijana Cohen Bramall kufanya kosa na Mpira kunaswa na N'Golo Kante aliemlisha Mfungaji Batshuayi.
Hadi Mapumziko, Arsenal 0 Chelsea 2.
Dakika ya 49 Chelsea walipiga Bao la 3 Mfungaji akiwa Batshuayi baada kupokea Pasi ya Marcos Alonso.
Bao hizo 3-0 zlidumu hadi mwisho.
Timu hizi zitakutana tena katika Siku 15 zijazo huko Wembley Stadium Jijini Lgao ondon kwenye Mechi ya fungua dimba Msimu Mpya ya kugombea Ngao ya Jamii.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Arsenal: Ospina, Maitland-Niles, Mertesacker, Monreal, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka, Bramall, Ozil, Iwobi, Lacazette.
Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Kante, Fabregas, Alonso, Willian, Batshuayi, Pedro.
Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
Arsenal
13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]
15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]
19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup [1-1, Penati 3-2]
22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing) (3-0]
29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)
30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)
6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)
Chelsea
22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing [3-0]
25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)
29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)
6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)
 
 
 
 

BIRD’S NEST STADIUM, BEIJING – JUMAMOSI: NI MABINGWA CHELSEA NA ARSENAL!

>NI MECHI YA KIRAFIKI ILA WENGER ADAI ‘HAINA URAFIKI’!

ARSE CHE CHINAJUMAMOSI Saa 8 Dakika 40 Mchana, Saa za Bongo, Mabingwa wa England Chelsea watashuka Bird’s Nest Stadium Mjini Beijing Nchini kucheza Mechi yao ya kwanza kabisa ya kujiweka sawa na Msimu Mpya kwa kupambana na Arsenal ambao tayari wana Mechi 3 kibindoni.

Arsenal, wakiwa wamecheza Mechi 2 huko Australia na 1 Shanghai, China dhidi ya Bayern Munich waliyotoka Sare 1-1 na kushinda kwa Penati 3-2, wanatinga kwenye Mechi hii ikiwa ni Wiki 8 tu tangu wawabwage Chelsea kwenye Fainali ya FA CUP Uwanjani Wembley Jijini London.

Akiiongelea Mechi hii, Meneja wa arsenal Arsene Wenger ameeleza hii si Mechi ya Kirafiki ingawa rasmi inapaishwa kama Mechi ya Kirafiki.

Wenger atapata nafasi murua kumtesti Straika wake Mpya kutoka France Alexandre Lacazette kama ni kifaa hasa kwa sulubu za Timu za England.

Kwenye mtanange huu, kila Timu itawakosa Mastaa wao kadhaa.

Arsenal itawakosa Theo Walcott na Sead Kolasanic ambao ni Wagonjwa wakati Shkodran Mustafa na Alexis Sanchez bado hwajakumuika na Kikosi kwa sababu bado wako vakesheni baada ya kushiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara wakiwakilisha Nchi zao Germany na Chile.

Chelsea itawakosa Wachezaji wao Wapya Alvaro Morata na Antonio Ruddier huku pia Eden Hazard akiwa bado hajapona maumivu yake na Diego Costa akitemwa huku akihusishwa na kurudi Klabu yake ya zamani Atletico Madrid.

Pia Tiemoue Bakayoko hayumo akiuguza maumivu yake baada ya kufanyiwa Operesheni ya Goti mwishoni mwa Msimu uliopita.

Mwingine ambae atakosekana Chelsea ni Kiungo Nemanja Matic ambae hayumo kwenye msafara baada ya kuhusishwa na kuihama Klabu hiyo.

Lakini, Kikosini mwa Chelsea wamo Chipukizi Wanne ambao ni Jake Clarke-Salter, Fikayo Tomori, Marcin Bulka na Kyle Scott.

Pia yumo Straika wao mwenye Miaka 30 Loic Remy ambae hajasikika kwa muda mrefu sasa.

Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

Arsenal

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup (1-1, Penati 3-2)

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)

Chelsea

22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing

25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: ARSENAL YAIBWAGA BAYERN KWA PENATI 3-2!

ARSRNAL BAYERNBAO la kusawazisha la Dakika ya 94 la Alex Iwobi liliwapa Sare ya 1-1 Arsenal walipocheza na Bayern Munich huko Shanghai na kisha kupata ushindi wa 3-2 kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano kwenye ya kugombea International Champions Cup.ARSENAL BAUERN2
Bayern ndio waliopata Bao la kuongoza kwa Penati ya Dakika ya 9 iliyofungwa na Robert Lewandowski aliemchambua Kipa Petr Cech.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia Ainsley Maitland-Niles kumsukuma Juan Bernat.
Bao hilo lilidumu hadi Dakika 90 kugonga na kwenye Dakika ya 4 ya muda wa Majeruhi Iwobi akaisawazishia Arsenal kwa Kichwa alipounga Krosi ya Aaron Ramsey.
Hadi mwisho Arsenal 1 Bayern 1.
Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Bayern kukosa 3 zilizopigwa na David Alaba, Sanches and Bernat wakati Ramsey, Nacho Monreal na Iwobi wakiifungia Arsenal.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Arsenal XI: Petr Cech; Krystian Bielik, Per Mertesacker, Nacho Monreal, Ainsley Maitland-Niles; Francis Coquelin, Granit Xhaka, Sead Kolasinac, Mesut Ozil; Danny Welbeck, Alexandre Lacazette.
Bayern Munich XI: Tom Starke, Rafinha, Juan Bernat, Mats Hummels, David Alaba; Corentin Tolisso, Franck Ribéry, Javi Martínez, Thomas
Arsenal – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup (1-1, Penati 3-2)

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)