FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU: MCHEZAJI BORA DUNIANI RONALDO APIGA BAO REAL IKITINGA FAINALI!

RONALDO-CLUBAMERICAMABINGWA wa Ulaya Real Madrid wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo Leo wametinga Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko Yokohama International Stadium Nchini Japan kwa kuwachapa Club America Bao 2-0.

Bao za Real, ambao sasa wamefikisha Mechi 36 mfululizo bila kufungwa, zilifungwa na Karim Benzema na Cristiano Ronaldo katika Dakika za 47, kipindi cha Kwanza, na 93.

Lakini Bao la Pili, ambalo alifunga Ronaldo, ilibidi lipasishwe na VARs, Msaada wa Teknolojia ya Video, ambalo liliangaliwa kwenye Video pembezoni mwa Uwanja kama lilikuwa Ofsaidi au la.

Hatimae Bao hilo likakubaliwa.

Kwenye Fainali, hapo Jumapili, Real watavaana na Kashima Antlers ambayo ni Klabu Wenyeji kutoka Japan.

Ikiwa Real watatatwaa Taji hili basi litakuwa ni Kombe la Dunia lao la Pili katika Kipindi cha Miaka Mitatu.

++++++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

KOMBE LA DUNIA KWA KLABU:
-
Kombe la Dunia kwa Klabu hushirikisha Klabu Bingwa za Mabara 6 ya Mashirikisho ya Soka Wanachama wa FIFA pamoja na Klabu Bingwa ya Nchi Wenyeji Japan.

VARs:

- Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

Mfumo wa Video kusaidia maamuzi ya Marefa Uwanjani, VARs [Video Assistant Referes] umefanyiwa Majaribio rasmi ya FIFA kwa mara ya kwanza katika Mechi ya Kimataifa hapo Septemba 1 wakati Italy ilipocheza na France huko Bari.

Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kutizama na kuliptia tukio na kutoa uamuzi wake.

Ama Refa huyo anaweza kumuomba Refa Msaidizi kulipitia tukio ili ampe ushauri.

++++++++++++++++++++++++++++++

Kabla ya Fainali hapo Jumapili, itakuwepo Mechi ya kusaka Mshindi wa 3 kati ya Atletico Nacional na Club America.

VIKOSI:

Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Navas; Carvajal, Varane, Nacho, Marcelo; Kroos, Casemiro, Modric; Lucas, Benzema, Ronaldo.

Akiba: Yanez, Casilla, Pepe, Ramos, James, Coentrao, Kovacic, Mariano, Asensio, Morata, Isco, Danilo.

America (Mfumo 4-3-3): Munoz; Alvarado, Valdez, Goltz, Aguilar; Samudio, Da Silva; Sambueza; Ibarra, Peralta, Romero.

Akiba: Gonzalez, Buron, Pimental, Guemez, Martinez, Arroyo, Leon, Mares, Guerrero, Quintero, Alvarez.

REFA: Enrique Patricio Cáceres [Paraguay]

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU

Ratiba/Matokeo

**Saa za Bongo

Alhamisi Des 8

Kashima Antlers 2 Auckland City 1

Jumapili Des 11

Robo Fainali

Jeonbuk Hyundai Motors 1 América 2

Mamelodi Sundowns 0 Kashima Antlers 2

Jumatano Des 14

Mshindi wa 5

Jeonbuk Hyundai Motors 4 Mamelodi Sundowns 1

Nusu Fainali

Atlético Nacional 0 Kashima Antlers 3

Alhamisi Des 15

Club América 0 Real Madrid 2

Jumapili Des 18

Mshindi wa 3

1000 Atletico Nacional v Club America

Fainali

1300 Kashima Antlers v Real Madrid