MWENZAKE MBWANA SAMATTA KUTUA LEICESTER CITY!

LEICESTER-NDIDI-SAMATTA2MABINGWA wa England Leicester City wameshaafiki dili ya kumsaini Wilfred Ndidi kutoka Klbu ya Genk ya Belgium kwa Malipo ya Pauni Milioni 15 yenye nyongeza ya Pauni Milioni 3 juu.

Ndidi, Mnigeria mwenye Miaka 20 ambae ni Kiungo, tayari amefanyiwa awamu ya kwanza ya upimwaji afya ambao unatarajiwa kukamilika kabla Januari 1 ili Uhamisho wake ukamilike.

Hivi sasa Leicester wamemwombea Mchezaji huyo Kibali cha Kazi cha Uingereza na mara baada ya hilo kwisha Mabingwa hao wanatarajiwa kumtangaza rasmi kutua King Power Stadium.

Meneja wa Leicester, Claudio Ranieri, anamchukulia Ndidi kama ni mbadala halisi wa Kiungo kutoka France, N’Golo Kanté, aliehamia Chelsea mwanzoni mwa Msimu.

Msimu wote huu Leicester wameyumba sana kwa kumkosa Kiungo Kante na ujio huu wa Ndidi utawafanya wajinasue toka karibu na mkia wa EPL, Ligi Kuu England, ambako Nafasi ya 16.

Leicester pia wapo Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambako watacheza na Sevilla ya Spain.

Ndidi ni Mzaliwa wa Lagos, Nigeria na kipaji chake kuvumbuliwa na Msaka Vipaji wa Manchester United, Roland Janssen, ambae alimwona kwenye Mashindano ya Vijana Mwaka 2013.

Mwaka 2015, Ndidi akajiunga na Genk, Klabu ya Belgium ambayo ni maarufu Tanzania kwa vile Straika na Nahodha wa Nchi hiyo, Mbwana Samatta, anaichezea.

Akiwa na Genk, Ndidi amechezea Mechi 62 za Ligi na kufunga Bao 4.