MOURINHO YU CROATIA KUMFUATILIA PERISIC, NAE GRIEZMANN KUIGHARIMU MAN UNITED €100M!

PATA FUPI ZA LEO:

GRIEZMANN-PERISICMOURINHO APAA KWENDA CROATIA

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amepaa kwenda Croatia kwa kile kinachodaiwa kuharakisha kumsaini Staa wa Inter Milan Ivan Perisic.

Habari toka huko England zimedai Mourinho yuko huko Zagreb ambako Leo Usiku Croatia wako kwao kuivaa Ukraine kwenye Mechi ya Kundi lao la kusaka kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Huku Chelsea na Liverpool pia zikidaiwa kumwinda Perisic ambae Dau lake linadaiwa kuwa Pauni Milioni 35, Mourinho ndie anapewa nafasi kubwa kumchota Mchezaji huyo wa Croatia kutokana na uhusiano wake mzuri sana na Wakala wake Predrag Mijatovic.

Perisic, mwenye Miaka 28, ana uwezo mkubwa wa kucheza kama Kiungo Mshambuliaji na nafasi zote za Fowadi.

MAN UNITED TAYARI KULIPA €100M KUMCHUKUA GRIEZMANN!

ZIPO Ripoti nzito kuwa Manchester United wanakaribia kuimaliza Dili ya kumsaini Mfaransa Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid.

Ripoti hizo zimedai Man United italipa Euro Milioni 100 kumsaini Griezmann mwenye Miaka 26.

++++++++++++

JE WAJUA?

Antoine Griezmann: Ni pekee Lionel Messi (Bao 168) na Cristiano Ronaldo (Bao 167) ndio wamefunga Mabao mengi kwenye la La Liga kupita Griezmann (Bao 84) tangu Agosti 2012.

++++++++++++

Ripoti hizo zimefafanua kuwa Jose Mourinho na Man United hawatakuwa na shida kulipa Dau kubwa kwa Griezmann na kumpa Mshahara mkubwa kwa vile inatarajiwa Wayne Rooney ataondoka mwishoni mwa Msimu na hivyo kuipunguzia Klabu hiyo zigo kubwa la Mshahara mkubwa wa Rooney.

SIR ALEX AIHIMIZA MAN UNITED KUBEBA EUROPA!

Manchester United wanapaswa kutilia mkazo UEFA EUROPA LIGI Msimu huu ili kulipeleka Old Trafford Taji ambalo hawajawahi kulibeba na kwa kufanya hivyo kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Msimu ujao.

Hiyo ni rai ya Meneja wao wa zamFERGIE-UBINGWAani Sir Alex Ferguson.

Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 5 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Liverpool ingawa wao wana Mechi 2 mkononi.

Kama wakimaliza Ligi wakiwa ndani ya 4 Bora watafuzu kucheza UCL Msimu ujao lakini Sir Alex Ferguson, ambae alikuwa Meneja wa Man United kwa Miaka 27, anaamini njia nzuri kwao kutinga UCL ni kupitia EUROPA LIGI.

Ameeleza: “Ukweli ni kuwa hatujawahi kutwaa EUROPA LIGI, hatukushinda UEFA CUP kabla ya hapo. Na sasa tupo njia njema, si hakika, lakini ipo nafasi kubwa. Bado ni Taji kubwa. Ukilitwaa unacheza CHAMPIONZ LIGI. Motisha ni kubwa kwa kutimiza hilo!”

Klabu za England hazijatwaa Taji lolote la Ulaya tangu Mwaka 2012 Chelsea walipochukua Ubingwa wa UCL na safari hii Timu zilizobaki kwenye michuano ya Ulaya Hatua ya Robo Fainali ni Mabingwa wa England Leicester City ambao wako UCL na wataivaa Atletico Madrid na Man United walio EUROPA LIGI na watapambana na Anderlecht.

Ferguson, ambae alibeba UCL mara 2 na Kombe la Washindi Ulaya akiwa na Man United, amebainisha kuwa mafanikio Ulaya ni mzunguko.

Ferguson, mwenye Miaka 75, ameeleza: “Miaka ya 70 na 80, Ajax na Bayern, Miaka ya 80, Liverpool, 90 ni AC Milan na baadae England ilitawala. Kwa sasa ni Timu za Spain. Na wao ni bora, ndio maana wanashinda!”

WENGER ARUKA TETESI ZA KWENDA PSG, ADAI NI ‘HABARI FEKI!’

WENGER-HATIMAArsene Wenger amezikanusha habari kuwa amepewa Mkataba kujiunga na Mabingwa wa Nchini kwao France, Paris Saint-Germain.

Wenger, mwenye Miaka 67, anamaliza Mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa Msimu huu lakini tayari Klabu hiyo ishamwekea Mezani Mkataba Mpya wa Miaka Miwili na yeye Juzi, mara baada ya kutandikwa 3-1 na West Bromwich Albion huko The Hawthorns, kutamka tayari ashaamua nini hatima yake na uamuzi huo utakuwa bayana hivi karibuni.

Kipigo hicho cha Arsenal ni chao cha 4 katika Mechi zao 5 za mwisho za EPL, Ligi Kuu England na kimewashusha hadi Nafasi ya 6.

Hali hiyo imewagawanya mno Mashabiki wa Arsenal na kumekuwa na Maandamano ya Makundi Mawili kati yao, moja likimpinga na jingine kumsapoti.

Hivi karibuni Wenger alikaririwa akisema kuwa ikiwa ataondoka Arsenal basi atatua Klabu nyingine kuendelea na kazi na PSG, Klabu ya Nchini kwao na Tajiri, inaonekana ni muafaka kwake hasa baada ya Meneja wao Msimu huu, Unai Emery, kuonekana kuyumba.

Lakini Wenger hii Leo amekanusha uvumi huo kwa kutamka: “Ni uvumi wa uongo, ni kile kinachoitwa ‘Habari Feki’! Naikanusha rasmi, si kweli!”

Mbali ya kuzorota hivi karibuni, na hasa kubamizwa Jumla ya Bao 10-2 na Bayern Munich katika Mechi 2 na kutupwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Wachambuzi huko England wamesisitiza Wenger atasaini Mkataba mpya na kubaki Arsenal.

Pengine tamko la kubakia huko Emirates linasubiri nini kitajiri kwa matokeo ya Uwanjani ya Mwezi Aprili ambao wanauanza kwa mtanange mkali wa EPL hapo Aprili 2 wakiwa Nyumbani kuwavaa Man City ambao pia watapambana nao tena huko Wembley Stadium kwenye Nusu Fainali ya FA CUP hapo Aprili 23.

BORO YAMTIMUA KARANKA, SWAHIBA WA MOURINHO!

MOU-KARANKAAitor Karanka ametimuliwa Umeneja na Middlesbroughambayo ni maarufu kama Boro.

Karanka, Raia wa Spain mwenye Miaka 43, ameondolewa Asubuhi hii akiiacha Timu hiyo aliyodumu nayo kwa Miaka Mitatu na Nusu ikiwa Nafasi ya 19 kati ya Timu 20 za EPL, Ligi Kuu England.

Boro hawajashinda katika Mechi 10 za Ligi, mara ya mwisho ikiwa Desemba 17, huku wakifunga Bao 3 tu katika kipindi hicho.

Aliekuwa Msaidizi wa Meneja, Steve Agnew, ndie atakaimu nafasi ya Karanka.

Kutimuliwa kwa Karanka, ambae ni swahiba mkubwa wa Meneja wa Man United, Jose Mourinho, Timu ambayo Boro wataivaa katika Mechi ya Ligi inayofuata, kulitangazwa kwenye Tovuti ya Klabu hiyo Asubuhi hii.

Karanka na Mourinho walikuwa wote huko Real Madrid baada ya Mourinho kumteua kuwa Msaidizi wake Juni 2010.

Licha ya kusuasua, Karanka aliamini atarekebisha mambo kwenye Mechi zao 11 za Ligi walizobakisha na hasa alipata imani hiyo baada ya kucheza vizuri Mechi yao ya mwisho walipopigwa 2-0 na Man City kwenye Robo Fainali ya FA CUP Jumamosi iliyopita.

 

 

PEP GUARDIOLA: ‘BILA KOMBE MSIMU WA MANCHESTER CITY UMEFELI!’

PEP-TAJIPep Guardiola amekiri kuwa ikiwa kwenye Msimu wake huu wa kwanza na Manchester City utaisha bila kutwaa Kombe lolote basi utakuwa umefeli.

Akiwa na mafanikio makubwa kwenye Klabu za Barcelona na Bayern Munich, Guardiola alitegemewa kupata mafanikio makubwa alipotua City lakini matarajio ya kutwaa Ubingwa wa England yanafifia wakiwa nyuma ya Vinara wa Ligi Chelsea kwa Pointi 10 huku Mechi zimebaki 11.

Hata hivyo, Manchester City bado wamo kwenye FA Cup na UCl, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Guardiola ameeleza: “Kama sipati Kombe sitakuwa hapa muda mrefu! Bila Kombe hautakuwa Msimu mzuri! Nilijua hilo tangu Agosti. Kuwa Meneja kunategemea mafanikio!”

Guardiola ametoboa kuwa akiwa na Bayern hakutwaa UCL bali alitwaa Ligi mara 3 na hilo kuonekana ni maafa.

Ameeleza: “Nilitwaa Ubingwa wa Ligi mara 3 mfululizo, tulibeba Vikombe Viwili kati ya Vitatu na kufika Nusu Fainali na Fainali ya vingine na hayo kuonekana ni maafa!”