WENGER: ‘BAO ZA CITY OFSAIDI..!! MAREFA WANALINDWA KAMA SIMBA WA ZOO!’

WENGER-BAOZACITY-OFSAIDIMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amekuja mbogo baada ya Timu yake Jana kuongoza 1-0 na kisha kupigwa 2-1 na Manchester City huko Etihad katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Wenger amemtuhumu Refa wa Mechi hiyo Martin Atkinson kuizawadia City Bao 2 za Ofsaidi mwishoni mwa Wiki mbaya kwa Arsenal ambao wamechezea vichapo viwili mfululizo baada ya Majuzi kupigwa 2-1 na Everton huko Goodison Park na kutupwa Nafasi ya 4 kwenye EPL wakiwa nyuma ya Liverpool, Man City na Vinara Chelsea.

Arsenal walitangulia kufunga katika Dakika ya 5 kwa Bao la Theo Walcott ambalo lilidumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Man City walikuja wapya na kuirudisha Arsenal nyuma na Dakika ya 47 kusawazisha kwa Bao la Leroy Sane.

Bao la ushindi kwa City lilifungwa Dakika ya 71 na Raheem Sterling huku David Silva akionekana kuwa Ofsaidi akimkaribia Kipa Petr Cech.

Baada ya Mechi hiyo na City, Wenger alieleza: “Maamuzi yalitupinga sisi. Zile Goli 2 zilikuwa Ofsaidi na hicho ni kitu kigumu kukikubali katika Mechi kubwa kama ile. Sasa imetosha kwa sababu Msimu mzima tunapata maamuzi mabovu dhidi yetu na nimeangalia zile Gole, zote Ofasaidi!”

Aliongeza: “Lakini, kama inavyojulikana vilivyo, Marefa wanalindwa sana, kama Simba kwenye Zoo, hivyo inabidi tuishi tu na maamuzi yao. Nataka walindwe sana. Lakini wakifanya maamuzi sahihi itakuwa vyema zaidi!”

Mechi inayofuata ya EPL kwa Arsenal ni Jumatatu Desemba 26 wakiwa kwao Emirates kucheza na West Bromwich Albion.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool  

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City          

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea