JURGEN KLOPP ATAKA UBINGWA NA LIVERPOOL MSIMU HUU!

LIVERPOOL-KLOPP-MAZOEZINIMENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp amesema Timu yao inawania Ubingwa Msimu huu na hawajali kufeli kwa Klabu hiyo Miaka iliyopita.

Liverpool hawajatwaa Ubingwa wa England tangu Msimu wa 1989/90 na Msimu huu, baada ya Mechi 17 kati ya 38, wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.

Akiongea kabla mfululizo wa Mechi zao za Kipindi hiki cha Krismasi kuelekea Mwaka Mpya ambapowatacheza Mechi 3 ndani ya Siku 7 kuanzia Jumanne Desemba 27 hadi Januari 2.

Liverpool wataanza na Stoke City Jumanne Desemba 27 huko Anfield, kisha Man City hapo Jumamosi Desemba 31 pia Anfield na Januari 2 kucheza Ugenini na Sunderland.

Klopp amesisitiza Klabu ipo imara kupigania Ubingwa Msimu huu na kuwataka Wachezaji na Mashabiki kutilia mkazo Msimu huu na kutofikiria nini kilitokea kwa Misimu 26 iliyopita.

Klopp ameeleza: “Hatupo Miaka 25 iliyopita. Tupo wakati huu. Sisi ndio Kizazi!”

Aliongeza: “Ingawa tuliwapenda mno Watu walioitengeneza Klabu hii, lakini hatungenezi kazi zao. Inabidi sisi tufanye kazi yetu!”

EPL - MECHI MFULULIZO KIPINDI CHA KRISMASI KUELEKEA MWAKA MPYA:

EPL-XMAS-NEWYEAR

Klopp amewataka Wachezaji kutimiza wajibu wao kwani wapo vizuri na Klabu yao ni kubwa.

Msimu huu, Liverpool imeshawafunga Chelsea na Arsenal ambao wapo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa lakini pia wamefungwa na Timu ‘dhaifu’ kama vile Burnley na Bournemouth.

Klopp ametamka: “Mpzaka sasa tumecheza Msimu mzuri lakini kuwa Bingwa pia unahitaji uwe na bahati na usipate majeruhi!”