RUFAA KADI NYEKUNDU: YA FEGHOULI YAFUTWA, FERNANDINHO YAMGANDA – KIFUNGO MECHI 4!

>BOURNEMOUTH NAO WAKATA RUFAA NYEKUNDU YA MCHEZAJI WAO MECHI NA ARSENAL! 

WESTHAM-MANUNITED-JONES-FEGHOULIFA, Chama cha Soka England, Leo kimeifuta Kadi Nyekundu ya Kiungo wa West Ham Sofiane Feghouli aliyopewa kwenye Mechi na Manchester United Juzi lakini Kiungo wa Manchester City Fernandinho atatumikia Kifungo cha Mechi 4 kufuatia kushindwa Rufaa ya kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Majuzi wakicheza na Burnley.

Feghouli, Mchezaji kutoka Algeria, alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean Jumatatu Usiku lakini baada ya hatua hii ya FA sasa atakuwa huru kuichezea West Ham Ijumaa Usiku wakicheza Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP na Manchester City.

Siku hiyo, Fernandinho wa Man City ataanza kutumikia Kifungo chake cha Mechi 4.

Mbrazil huyo alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumrukia Miguu Miwili Johann Berg Gudmundsson wa Burnley na sasa atatumikia Kifungo cha Mechi 4 badala ya 3 za kawaida kwa vile hiyo ni Kadi Nyekundu yake ya Pili Msimu huu kwenye EPL, Ligi Kuu England.

Fernandinho pia alipewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya City na Borussia Mönchengladbach ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwezi Desemba na kumfanya awe amepewa Kadi Nyekundu 3 ndani ya Mechi 6.

WAKATI HUOHUO, Bournemouth imetangaza kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu kwa Mchezaji wao Simon Francis aliyopewa walipotoka Sare 3-3 na Arsenal Jumanne Usiku.